Mtunzi: Rumafrica
MAAGIZO: Hurusiwi kuangalia jibu kabla ya kumaliza kujibu maswali Yote. Msimamizi wetu ni Yesu Kristo. Unapojibu tuonyeshe umejibu swali la ngapi, kwa mfano 1(a) au 3(c). Mungu akubariki Sana
Producer Baraka
MASWALI KUTOKA KATIKA KITABU CHA LUKA 15-20
- Jambo gani lilitokea mpaka Yesu akasema, kutakuwa na furaha kwa
wenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwaajili ya wenye haki tisini na
kenda ambao hawana haja ya kutubu
- Malizia habari ya tajiri na maskini
a) Palikuwa na tajiri aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula siku zote kwa anasa. Na maskini mmoja jina lake..........................huwekwa mlangoni pake anavidonda vingi naye alitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule b) Hata mbwa wakaja wakamlamba............................ c) Ikawa yule masikini alikufa akachukuliwa na ............................. d) mpaka kifuani kwa........................ Yule tajiri naye akafa, akazikwa. e) Basi kule.............................. akainua macho yake aalipokuwa katika mateso, f) akamwona............................kwa mbali na g)......................... kifuani mwake h) akalia akasema,................................................. - Malizia sentensi hii .
a) Makwazo hayana budi kuja ila ole wake................................................
b) Jilindeni kama ndugu yako akikosa................................................
c) Imewapasa kumuomba Mungu siku zote, wala.................................... - Ni watu gani walisema Bwana tuongezee imani? Yesu aliwaambia nini hawa watu juu ya kuongezewa imani?
- Watu wenye ukoma walimwambia nini Yesu walipomuona kwa mbali, na Yesu alisema nini kwa hao wenye ukoma?
- Yule aliyepona ukoma alifanya nini kumtukuza Mungu?
- Yesu alimwambia nini Msamaria aliyepona ukoma baada ya kumtukuza?
- Yesu aliwajibu nini Mafarisayo walipomuuliza juu ya siku ya kuja ufalme wa Mungu?
- a)Taja jina la aliyetamani kumuona Yesu katika mji wa Yeriko na alikuwa mtoza ushuru.
b) Kwanini alihangaika kumuona Yesu?
c) Alifanya nini kumuona huyu Yesu, na kwanini alifanya hivyo?
- Baada ya Mafarisayo na waandishi kunung'unika wakisema, Mtu huyu
huwakaribisha wenye dhambi tena hula nao. Na aliweza kutoa mfano wa
kondoo aliyepotea (soma Luka 15:1-7)
- a) Lazaro b)vidonda c) malaika d) Ibrahimu e) kuzimu f) Ibrahimu g)
Lazaro h)Ee Baba Ibrahimu nihurumie , umtume Lazaro achovye ncha ya
kidole chake majini, aburudishe ulimi wangu, kwasababu ninateswa katika
moto huu
- a) mtu yule ambaye yaja kwasababu yake!
b) mwonye, akitubu msamehe
c) Msikate tamaa - Mitume, Yesu alisema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya
haradali mngeuambia mkuyu huu ng'oka ukapandwe baharini, nao ungewatii.
- Ee Yesu Bwana mkubwa uturehemu, alipowaona akawambia, Enendeni mkajionyeshe kwa makuhani
- Alimtukuza Mungu kwa sauti, akaanguka kifudifudi miguuni pake akamshukuru naye alikuwa Msamaria
- Enenda zako imani yako imekuponya
- Ufalme wa Mungu hauji kwa kuchunguza, wala hawatasema tazama, upo huku au kule, kwa maana tazama ufalme wa Mungu uko ndani yenu
- a) Zakayo.
b) Kwasabau alikuwa mfupi sana na alitamani kumuona Yesu ni wa namna gani
c) Alipanda juu ya mkuyu apate kumona kwa kuwa atakuja kupita njia ile
Comments