RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHEMASHA BONGO NA BIBLE KITABU CHA YOHANA 2

MASHARTI: Jibu maswali yote bila ya kusoma Biblia au kuangalia majibu yaliyoandaliwa hapo chini. Ukifanya vinginevyo utakuwa umetenda dhambi.
MSIMAMIZI WA CHEMSHA BONGO: Yesu Kristo, Mungu na Roho Mtakatifu. Ninakuomba usiangalizie mpaka umemaliza maswali yote. Tutumia kwa Watsap majibu yako kwa namba hii +255 715 851 523.
MTUNZI: Rumafrica For All Nations

SarahMvungi - Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, MC, Mwinjilisti, Mwigizaji wa Filamu, Nesi wa TMJ Dar es Salaam Tanzania. Wasiliana naye kwa simu +255 717 308 282

MASWALI
  1. Taja mji ambao Yesu na wanafunzi wake pamoja  na mama yake walialikwa katika arusi?
  2. Mama yake Yesu alimuomba nini Yesu pale arusini afanyiwe baada ya kuona wenyeji wametindikiwa?
  3. Yesu alitumia nini kupata divai pale arusi katika mji wa Galilaya huko Kana?
  4. Mabalasi aliyotumia Yesu Kristo kupata Divai yalitumika kama nini kwa Wayahudi?
  5. Yesu aliwaambia wanafunzi wafanye nini kupata Divai kwa kutumia mabalasi, na wampelekee nani ayaonje?
  6. Mkuu wa meza alimwambia nini bwana arusi juu ya divai iliyogeuzwa Yesu kutoka mabalasi na kuwa divai?
  7. Siku ya Pasaka ilivyokaribia Yesu alikwea kuelekea wapi?
  8. Vitu gani Yesu aliviona alipokwea kuelekea Yerusalemu?
  9. Yesu aliwaambia nini wale waliokuwa wakifanya biashara katika hekalu?
  10. Yesu aliwaambia ni muda ngapi alitalijenga hekalu la Baba baada ya kulivunja?
  11. Wayahudi walimwambia Yesu ni kwa muda gani wanafikiri Yesu angelijenga hekalu baada ya kulibomo)
  12. Yesu alikuwa akimaanisha nini juu ya kulijenga hekalu la Baba baada ya kulibomoa?
  13. Kwanini Yesu hakujiaminisha kwa Wayahudi hasa kipindi kile cha pasaha na hakutaka kushuhudia habari za wanadamu?
MAJIBU
  1. Mji wa Galilaya huko Kana (Yohana 2:1)
  2. Divai(Yohana 2:3)
  3. Mabalasi sita ya mawe (Yohana 2: 6)
  4. Kutawadha kutokana na desturi ya Wayahudi (Yohana 2:6)
  5. Wajalize mabalasi maji, wampelekee mkuu wa meza ayaonje (Yohana 2:8-9)
  6. Kila mtu wa kwanza huandaa divai iliyo njema, hata watu wakishakunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu, Wewe umeweka divai njema hata sasa. (Yohana 2:10)
  7. Yerusalem (Yohana 2:13)
  8. Aliona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa na wengine kuvunja fedha za wenye kuvunja fedha. (Yohana 2:14-16)
  9. Yaondoeni haya msifanye nyumba ya Baba yangu nyumba ya biashara. (Yohana 2:16)
  10. Siku tatu (Yohana 2:19)
  11. Miaka 46 (Yohana 2:20)
  12. Alimaanisha hekalu la mwili wake (Yohana 2:21)
  13. Yesu aliwajua wote (Wayahudi) nia yao kwa maana Yeye mwenyewe alijua yaliyo ndani ya mwanadamu (Yohana 2:24)

Comments