Christina Mbilinyi ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Mwimbaji huyu ni mmoja kati ya waimbaji walioweza kuleta muamko wa uimbaji nchini Tanzania kwa nyimbo zake zilizomo katika albamu yake ya NASUBIRI BARAKA. Mungu alimpa neema ya uimbajiya kutunga wimbo huu ambao umefanyika baraka kwa walio wengi. Kuna baadhi ya watu wametamani kuingia katika uimbaji kutoka na uimbaji wake. Wimbo huu unasemekana ni wimbo ambao utakaa sana vichwani mwa watu bila kuisha makali yake yaani kuchuja kutokana na ujumbe uliomo na jinsi Mungu alivyoupa kibali masikioni mwa watu.
Christina Mbilinyi
Christina Mbilinyi kwa kabila ni Mkinga, na alishawahi kuwa mwalimu wa kwaya mkoani Mbeya kabla hajawa mwimbaji binafsi. Waimbaji wenzake katika kwaya aliyokuwa akifundisha walitokea kumpenda sana kwa unyenyekevu wake na utungaji wake wa nyimbo. Baadhi ya wanakwaya wenzake waliweza kuinuka kiuimbaji kutokana na matunda ya mwimbaji huyu.
Christina Mbilinyi
Baada ya kuishi Mbeya kwa muda mrefu na kuwa mwalimu wa nyimbo za Injili, aliamua kuhamia jijini Dar es Salaam na kuwa mwimbaji binafsi, na hii ilitokana na kubadilisha mazingira aliyoyazoea na kwenda mazingira mengine kutafuta riziki. Christina Mbilinyi kutokana na karama yake ya uimbaji hakuishi kutafuta maisha bali alikumbuka kile kitu ambacho Mungu ameweka ndani yake na akaamua sasa kuwa "seriuos" na kazi ya Mungu na kusimama kama yeye kwaajili ya kazi ya Mungu, ndipo alipoaamua kuwa mwimbaji binafsi.
Christina Mbilinyi
Mungu aliweza kumuwezesha kuingia studio na kufanya albamu yake ya kwanza iliyoenda kwa jina la NASUBIRI BARAKA ambaye ilimtambulisha na kujulikana na watu wengi sana. Kwa hivi sasa ameachia albamu yake mpya ya MTAZAMO WAKO yenye nyimbo nane (8) ambazo ni Nimekubali, Wahangaika, Napenda kushukuru, Si Shwari, Nifundishe, Yesu wa Kusifiwa. Albamu yake imerekodiwa JB Studio, Double B na PG Production. Katika albamu hii kuna watu ambao wameshiriki kuimba ambao ni Silas Mbise, David, na wengine ambao utawasikia ukiipata kazi hii. Nyimbo zote zimetungwa na yeye mwenye-Christina Mbilinyi.
Christina Mbilinyi ambaye kwa sasa anaabudu katika kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa, na unaweza kuwasiliana naye kwa simu +255 719 009 543.
Rumafrica iko katika harakati za kumtafuta Christina Mbilinyi kufanya naye mahojiano kujua mengi kutoka kwake kihuduma na maisha yake ya kawaida. Endelea kufuatilia mahojiano yetu