RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA CHEMSHA BONGO NA BIBLE

ONYO: Hurusiwi kuangalia majibu kabla hujajibu. Roho Mtakatifu ndiye msimamizi wa Mtuhani huu. Usiibie kwa jina la Yesu Kristo.
Maswali yaatoka Yohana 1
Mtunzi:Rulea Sanga

Joyce Ombeni: Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania

MASWALI

  1. Malizia aya hii
    Hapo mwanzo kulikuwapo na Neno, naye Neno alikuwa (a) .............................Huyo (b)....................alikuwa kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa Huyo. Hata pasipo Yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulikuwamo c)...................................... ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa d)................................., wala giza halikuweza.
  2. Ni nani aliyetumwa kutoka kwa Mungu, ambaye alikuja kwa ushuhuda ili aishuhudie ile nuru wote wapate kuamini kwa yeye. Huyo hakuwa na ile nuru balia alikuja ashuhudie ile nuru?
  3. Biblia inasema Neno alifanyika mwili akakaa kwetu, ili sisi tuweze kuona nini?
  4. Taja baadhi vitu alizoshuhudia kuvitamka Yohana juu ya kuja kwa Yesu Kristo, pale alipopaza sauti yake?
  5. Ni watu gani walitumwa kumuuliza Yohana kujua kama yeye ni Yesu Kristo, na walitumwa na nani?
  6. Yohana alipoulizwa na Makuhani na Walawi kuwa Yeye ni nani wakitaka kujua kama atajiita ni Yesu Kristo, aliwajibuje?
  7. Yohana aliwajibu wale Makuhani na Walawi kuwa yeye siye Kristo bali ni nani?
  8. Njia gani Yohana alitumia kubatiza watu?
  9. Yesu alibatiza kwa njia gani?
  10. Toa maana ya neno Rabi
  11. Taja majina mawili ya watu waliomsikia Yohana akiwataka kumfuata Yesu
MAJIBU
  1. a)  Mungu  b) Mwanzo c) Uzima d) gizani (Yohana 1:1-5)
  2. Yohana (Yohana 1:6)
  3. Utukufu kama wa Mwana pekee wa atoakaye kwa Baba (Yohana 1:14)
  4. i) Ajaye nyuma yangu (Yohana) amekuwa mbele yangu kwa maana alikuwa kabla yangu
     ii) Katika utimilifu wake sisi sote tulipokea neema juu ya neema
     iii) Hakuna mtu aliyemuona Mungu wakati wowote; Mungu mwana wa pekee aliye katika kifuacha Baba huyu ndiye aliyemfunua(Yohana 1:15-18)
  5. Waliotumwa ni Makuhani na Walawi, waliowatuma ni Wayahudi (Yohana 1:19)
  6. Mimi siye Kristo. Yohana 1:20
  7. Mimi ni sauti ya mtu aliye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena Nabii Isaya. (Yohana 1: 23
  8. Maji (Yohana 1:26)
  9. Roho Mtakatifu (Yohana 1:33)
  10. Mwalimu (Yohana 1:38)
  11. Andrea na Simoni Petro

Comments