RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA EFATHA MWENGE: SHIKA TUMAINI BILA KUKATISHWA TAMAA

Rumafrica ilibahatika kuhudhuria ibada ya pili inayoanza saa 4:00 asubuhi - 7:00 mchana katika kanisa la EFATHA Mwenge jijini Dar es Salaam kwa mtumishi wa Mungu Nabii na Mtume Josephate Mwingira na kujifunza mengi kwa kupitia mchungaji wa kanisa hilo ambaye jina sikubahatika kulipata. Ujumbe ulikuwa kama ifuatatavyo:

Nabii na Mtume Josepahte Mwingira (hakuhubiri Jumapili hii)

SHIKA TUMAINI BILA KUKATISHWA TAMAA NA HESHIMU MAMLAKA YA MUNGU NA YA WANADAMU WALIOPEWA MAFUTA NA MUNGU

Kesheni mkiomba kwasababu hamjui saa wala siku. Maisha ya mtu yamefananishwa na taa. Maisha ya mtu yanahitaji nuru na nuru ni Mungu. Mtu anaonekana na mafuta pale anapoamua kutomuacha Mungu na kusababisha na watu wengine kufurahia maisha yake. Mungu ni mwenye mamlaka kuliko wenye mwili.

Maisha ya mtu yanahitaji kuwa na hofu ya Mungu kwani Mungu anakutetea na mengi. Kumcha Mungu ni pamoja  na kuyaaangali hayo unayofanya serikalini au kanisani yanamfurahia jirani yako na sio kero. Mungu alimuumba binadamu sio kwaajili ya kumuudhi mwenzake bali awe na furaha kutoka kwako. 

Giza mara nyingi ndilo linaloleuta shida katika jamii ila nuru huleta amani kwetu. Pasipo na amani au mahali penye msiba mara nyingi huwa na huzuni lakini pale anapojitokeza Yesu katika eneo hilo furaha na amani hutawala.. Utakiwa kuwasha nuru ya Mungu hapoulipo, iwe kanisani, ofisini, shuleni n.k ili watu waokolewe.

Nuru ni njema na ndio maana hata taa ukiwasha usiku husababisha wadudu kufuata mwana. Mungu duniani haonekani kwa macho bali Mungu yupo duniani kwa kupitia watu wake. Taa yako ikizimika utajua pale utakapoona watu wanakukimbia hasa wale waliokupenda kipindi ulivyokuwa nuru kwao.

Kazi ya shetani ni kuharibu kazi ya mikono yetu. Popote alipo Yesu chochote unachoanzisha kinafufuka na kuwa hai kwani unapata msaada kutoka kwa Mungu wetu wa mbinguni. Mafuta yasipokuwepo katika taa haiwaki lakini ukiwa na taa yenye mafuta utapata mwanga, na sisi tuna taa yenye mafuta na ndio maana tunakuwa nuru kwa watu na watu wanaona matendo makuu katika maisha yetu.

Katika maisha yako anagalia una mafuta ya kutosha ili mwanga uzidi kuwaangaza. Kipindi cha kujaza mafuta ni hiki na sio kipindi kingine. Watumishi wa Mungu wanauza mafuta na wewe unatakiwa kujipanga kununua mafuta.. Mafuta hayapatikani kwa kusali sana bali kwa kutekeleza sheria za Mungu.

Tusome Warumi 13:1-2, kila mtu atii mamlaka. Mafuta yanapokuwepo unaweza kutambua mipaka yote. Kila mtu aheshimu mamlaka. Kuna aina za mamlaka

MAMLAKA YA WANADAMU NA MAMLAKA YA MUNGU
Katika mamlaka ya wanadamu kuna vitu vya giza  vinavyowataka kuwatumia. Na mamlaka hii hushambulia sana vijana. Kila mtu aiheshimu mamlaka na hasa wale waliopo katika mamlaka ya Mungu na wamepakwa mafuta na Mungu.. Mamlaka iliyokuwa ya Mungu ndio inasababisha kuishi maisha ya amamni.

Ukinyamazisha mamlaka ambayo Mungu ameachia kwa watumishi wake, hukusababishia wewe kupata matatizo. Watumishi wa Mungu wakilia jambo kubwa linatokea na pengine kukumba.. Kila mtu aheshimu mamlaka ya Mungu kwani unapokumbwa na shida hapo ndipo kimbilio lako, na hii mamlaka imeamuliwa na Mungu.

Unaposema habari za Mungu, naye hufurahia. Mtu anapotaka kuleta ujinga akiona Neno la Mungu huwa mdogo. Cheo chako ulichonancho ni mamlaka ya Mungu aliyokupa. Mamlaka ya Mungu ni mamlaka iliyo kuu. Kama watafanya ujinga bila ya kutii mamlaka iliyokuu, mabaya yatawajia.

Mamlaka ya Mungu inataka kuona watu wanapona na vidonda na magonjwa n.k. Hata unapokuwa umefanikiwa sana usisahau mamlakahii kuu ya Mungu. Yoyote anayesema habari za ufalme wa Mungu, huna sababu ya kusema baya juu yake. Ukitaka Mungu akuheshimu, waheshimu watumishi wa Mungu hata kama wako daraja la chini kanisani kwako kama vile wahudumu wa kanisa.

SHUHUDA
Mariam Mwambuta: Kutoka Morogoro nilikuwa naumwa sana natetemeka, nikapata ganzi mwili mzima nikalazwa Hospitali nikiwa nimefumba macho Hospitali nikamwona Mtume na Nabii Josephati Elias Mwingira ametokea mbele yangu akanishika kifuani na mgongoni mwangu sikusikia alicho sema lakini nilisikia sauti ikiniambia umepona. Nilipofika nyumbani nilipata ganzi tena mwili mzima nikazidiwa zaidi, nilikuwa siwezi majirani zangu wakanitoa nje nilikuwa naita Yesu Yesu,


Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akanitokea tena akaniambia usiogope, baada ya muda kupita nikaona watu wananisukumia kwenye kaburi, mara Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akaja tena akasema nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na ng’e na nguvu zote za yule adui hakuna kitakacho nishinda , akaja akanichukua na kunivuta mkono wake wa kulia, mwili wangu ulikuwa una dalili zote za kuparalaizi nikaamua kuja Dar es salaam, ndipo nilikutana na Mtumishi wa Mungu Mchungaji Daudi Urio wa Efatha Mwenge akanileta kanisani Efatha, nilipofika kanisani nikakutana na somo katika kitabu cha Yohana 6:1..,linasema mkutano mkuu ulimfuta Yesu kwasababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alikuwa anafundisha somo hilo akasema aliye kuja anaumwa akifika kitandani atapata uponyaji wake, niliamini na kweli nilipo rudi nyumbani nikasema ninalala ili nipate uponyaji nilipo amka nikajikuta nimepona hakuna tena ile hali ya kuparalaizi. Namshukuru Mungu wa Efatha kwa matendo makuu aliyo nitendea.

MUNGU AKUBARIKI SANA

Comments