Rumafrica imekuletea CHEMSHA BONGO NA BIBLE kutoka katika kitabu cha Yohana 6. Huruhusiwi kuangalia majibu katika Biblia yako kabla ya kujibu maswali. Tumia akili yako kwanza ili ujipime ukoje katika Neno la Mungu.
MSIMAMIZI WA MTIHANAI HUU NI Roho Mtakatifu. Ni dhambi kuangaliziaEvelyn Kabwelile-Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania
MASWALI
1. Kitu gani kiliwafanya makutano kumfuata Yesu alipokwenda zake ng’ambo ya Bahari ya Galilaya?
2. Yesu alipokwea mlimani, alikuwa na akina nani?
3. Pasaka ilikuwa ni siku ya akina nani?
4. Yesu alimwambia nani alipoona mkutano mkuu wanakuja pale alipoinua macho yake na kusema, “Tununue wapi mikate ili hawa wapate kula”?
5. Kwanini Yesu aliuliza swali hili kwa wanafunzi wake, “Tununue wapi mikate ili hawa wapate kula”?
6. Ni nani kati ya wanafunzi wa Yesu aliyeweza kuona mikate kutoka kwa motto aliyekuwa na mikate mitano na shayiri na samamki wawili?
7. Baada ya Yesu kuwaketisha watu wapatao elfu tano na kuwapa mikate na samaki na kwapa kadiri ya walivyotaka, nao waliposhiba walikusanya mabaki ya mikate na samaki vikapu vingapi?
8. Ni akina nani walisema, “Hakika huyu ni Nabii Yule ajae ulimwenguni?”
9. Yesu alichukua uamuzi gani baada ya kuona watu wamepanga kuja kumshika ili wamfanye mfalme?
10. Yesu alimaanisha nini aliposema, “Baba”?
11. Tufanyaje ili kuzitenda kazi za Mungu?
12. Malizia semi hizi za Yesu Kristo
(i) Amini amini nawaambieni………………………….
(ii) Wote anipao Baba watakuja kwangu, wala yeyote ajaye kwangu…………………..
(iii) Hakuna ajae kwangu (Yesu) isipokuwa amejariwa na…………………….
13. Tufanyaje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu?
14. Chakula cha Mungu ni chakula cha namna gani?
15. (a) Yesu alishuka kutoka mbinguni ili afanye mapenzi kwa nani?
(b) Taja mapenzi ambayo Yesu alitumwa na Mungu kuyafanya hapa duniani?
16. Ni siku gani Yesu aliwaambia Wayahudi wasinung’unike juu ya Yeye kujiita ni chakula kilichoshuka kutoka mbinguni bali atawafufua na hakuna mtu ajae kwake asipovutwa kwa Baba aliyempeleka ulimwenguni?
17. Ni kitu gani anakipata Yule anayemwamini Mungu?
18. Yesu anasema yeye ni chakula cha uzima kilichoshuka kutoka wapi?
19. Ni hasara ganitunapata tusipokula mwili wa mwana wa Adam na kunywa damu yake?
20. Ni sehemu gani Yesu alisema maneno juu ya kula chakula chake ambacho kinatupa uzima wa milele na pia kunywa damu yake?
21. Ni chakula cha aina gani ambacho anasema tukila tutapata uzima wa milele?
MAJIBU
1. Kwasababu waliona ishara alizozifanyia wagonjwa (Yohana 6J1)
2. Wanafunzi (Yohana 6:3)
3. Wayahudi (Yohana 6:4)
4. Filipo (Yohana 6:5)
5. Kwasababu alitaka kuwajaribu kwa maana alijua mwenyewe atakalolitenda (Yohana 6:6)
6. Andrea nduguye Simoni Petro (Yohana 6:8)
7. Vikapu 12 (Yohana 6:13)
8. Ni wale watu waliona ishara alizofanya Yesu (Yohana 6:14)
9. Alienda mlimani Yeye peke yake (Yohana 6:15)
10. Mungu (Yohana 6:27)
11. Mwamini Yeye aliyetumwa na Yeye (Yohana 6:29)
12. (i) Sitamtupa kamwe (Yohana 6:37)
(ii)Baba yangu (Yohana 6:65)
13. Tumwamini Yeye aliyetumwa na Mungu (Yohana 6:29)
14. Chakula kitokacho mbinguni na kuwapa ulimwengu uzima (Yohana 6:30)
15. (a)Mapenzi Yake aliyempeleka (Yohana 6:38)
(b) Katika wote alionipa nisimpotezee hata mmoja bali nimfufue siku ya mwisho (Yohana 6:40)
16. Siku ya mwisho (Yohana 6:43)
17. Uzima wa milele (Yohana 6:47)
18. Mbinguni (Yohana 6:51)
19. Hakuna uzima ndani yetu, na hatafufuliwa siku ya mwisho (Yohana 6:54)
20. Katika Sinagogi huko Kaepernamu(Yohana 6:59)
21. Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu (Yohana 6:63)
Comments