Rumafrica kwa Neema na Rehema za Mungu ilibahatika tena
kuingia katika nyumba ya Bwana wetu Yesu Kristo katika kanisa la EFATHA mwenge
kwa Nabii na Mtume Josephate Mwingira siku ya Jumapili 24/05/2015 ibada ya pili
inayoanza saa 4:00 asubuhi na kumalizika saa 7:00 mchana. Nabii na Mtume
Josephate Mwingira aliweza kutufundisha juu ya “Roho wa Uweza” Somo hili
limenibariki sana na ndio maana nikaona ni vizuri nikushirikishe na wewe ili
uweze kujifunza kitu kutoka kwa Mtumishi wa Mungu.
Ndiye Roho atendaye furaha katika maisha yetu, mtu wa Mungu
lazima awe na nguvu ya Mungu. (Zakaria.6:1). Ukisoma kitabu cha Zakaria,
kulikuwa na farasi weusi, wekundu, weupe na wakijivu, kupitia hao farasi wanne
tunajifunza kuwa kuna makundi manne yatuonyeshayo uwezo wa Mungu. Kulikuwa pia
na magari ya vita manne, yenye farasi weusi,
weupe, wekundu, na wakijivu, walioenda Mashariki, Kaskazini Kusini na
Duniani kote. Wale walioenda kaskazini walituliza moyo wa Mungu, magari hayo
yalikuwa yanatoka katika vilima viwili.
Tusome Efeso 3:4, katika kitabu hiki tunaona magari yalitoka
mbele za Mungu na kwenda duniani kote.
Pia tunajifunza kuwa kulikuwa na milima na Milima hiyo ni
milima ya shaba. Tunajifunza mashuleni kuwa shaba haivunjiki bali hujikunja
kwahiyo kama watu wa Mungu tunatakiwa kuwa kama shaba ambao iko imara na
haikubali kuvunjika hata kama inapita katika misukosuko. Biblia inatupa
mwangaza na ndio maana Agano la kale na Agano jipya litatudumu milele na
lilikuwa likilenga maswala ya kitume na kinabii, kwahiyo Biblia ni nguzo la
muhimili wetu wa Kikristo. Tunahitaji kusoma Neno la Mungu na kusoma vitabu
mbalimbali kwaajili ya kujua mambo mengi ya Mungu.
TUONE MAANA ZA HAWA FARASI WANAOZUNGUMZIWA KATIKA KITABU CHA
ZAKARIA
FARASI WEKUNDU: Farasi hawa wanazungumnzia ukombozi, damu
itakayo kuokoa na kukutakasa.
FARASI WEUPE: Maana yake ni utakatifu
FARASI WEUSI: Maana yake ni uovu
FARASI WA KIJIVU: Maana yake ni msumari aliyopigiwa Yesu Kristo msalabani.
Farasi wanne wanabeba ujumbe mzima wa kile kilichotendeka, farasi wanne hao ni pepo wanne wa mbinguni.
TUONE MAANA YA PANDE NNE ZILIZOZUNGUMZIWA KATIKA KITABU CHA ZAKARIA
Upande wa kaskazini: Maana yake ni moyo wa mwanadamu. Yesu alibeba uovu wetu na kwenda nao msalabani ili kila amwaminiye asipotee ili apate wokovu na ndio maana tunaona farasi weupe wanamfuata. Yesu alibeba maovu yetu na akafa msalabani. Upande huu unaleta maajabu mengi sana.
FARASI WEUPE: Maana yake ni utakatifu
FARASI WEUSI: Maana yake ni uovu
FARASI WA KIJIVU: Maana yake ni msumari aliyopigiwa Yesu Kristo msalabani.
Farasi wanne wanabeba ujumbe mzima wa kile kilichotendeka, farasi wanne hao ni pepo wanne wa mbinguni.
TUONE MAANA YA PANDE NNE ZILIZOZUNGUMZIWA KATIKA KITABU CHA ZAKARIA
Upande wa kaskazini: Maana yake ni moyo wa mwanadamu. Yesu alibeba uovu wetu na kwenda nao msalabani ili kila amwaminiye asipotee ili apate wokovu na ndio maana tunaona farasi weupe wanamfuata. Yesu alibeba maovu yetu na akafa msalabani. Upande huu unaleta maajabu mengi sana.
Upande wa kusini:
(Farasi wa kijivu). Yesu alisulubiwa kusini mwa Yerusalemu, na baada ya hapo
wakampigilia msalabani. Na hayo yote Yesu alikubali ili wewe na mimi tupate
kuokolewa. Huu ni upenda wa ajabu sana, hakuna mwanadamu aliyewahi kufanya haya
yote aliyofanya Yesu ya kukubali kusulubiwa kwaajili ya kuokoa mioyo ya watu.
Lengo zima la kuteseka ni kukuweka wewe huru na kufurahia maisha yako ya
duniani na siku ile ya kufa kwako ukafurahie maisha ya mbinguni.
Dunia yote: Tendo la kumwaga damu lilisababisha dunia kumpenda Kristo, na sisi tukasamehewa maovu yetu, ka kupigwa kwake sisi tumeokolewa. Hapa ndipo ilipo nguvu ya Neno la Mungu. Tusome Ezekieli 47: Tunashuhudia sasa kuwa Yesu Kristo anajulikana duniani kote iwe mijini au vijijini jina la Yesu limetapakaa na kutamkwa vinywani mwa watu. Hata kama kuna watu wanampiga huyu Bwana Yesu lakini bado wanatambua kuwa kuna mtumishi wa Mungu aliweza kukubali kufa na hatimaye kufuka ambaye ni Yesu Kristo.
Upande wa Mashariki: Maji
yaliyotokea ubavuni mwa Yesu na hayo maji mtu anayesogelea anapata uponyaji. Na ndio maana
mtu akiombewa Mungu anafanya uponyaji ndani ya mtu Yule amabaye naumwa. Kwahiyo
maji ni uzima wetu.
Roho wa Uweza ni
lugha ya mafumbo na huyo Roho wa Uweza amejificha sana, na kumtafuta inahitaji
mtu aliyempenda Mungu, na kufanya kwa bidii kumtafuta Mungu. Tunaweza
kufananisha na pesa, unapokuwa na pesa unaificha sana mfukoni mwako au ndani ya
nyumba yako kwasababu kuipata fedha kunahitaji akili nyingi na juhudi zako.
MAMBO YANATOWEZA
KUTOKEA BAADA YA KUPOKEA WOKOVU
Ukisoma kitabu cha Yohana 1:12, ulipokubali kumpokea Kristo na kufanya toba na kusema Yesu utamtumikia, unakuwa farasi wa Yesu na yeye anakupenda. (Mathayo 11), Bwana anasema jitie nira, kwa hiyo farasi ukimtia nira maana unataka kumpanda na kumuongoza unakotaka kwenda. Na sisi tumefanyika farasi wa Yesu na dio maana tunaongozwa na Yeye na anatulisha na kutufisha kama vile farasi akishatumika anahitaji kula na kuvaa kwasababu ametii na amefanya kile ulichokuwa unataka afanye.
Ukisoma kitabu cha Yohana 1:12, ulipokubali kumpokea Kristo na kufanya toba na kusema Yesu utamtumikia, unakuwa farasi wa Yesu na yeye anakupenda. (Mathayo 11), Bwana anasema jitie nira, kwa hiyo farasi ukimtia nira maana unataka kumpanda na kumuongoza unakotaka kwenda. Na sisi tumefanyika farasi wa Yesu na dio maana tunaongozwa na Yeye na anatulisha na kutufisha kama vile farasi akishatumika anahitaji kula na kuvaa kwasababu ametii na amefanya kile ulichokuwa unataka afanye.
Roho ya uweza inafanya maajabu kwa mtu, wokovu ni Roho
ambayo inatembea katika Roho wa uweza, na husababisha watu kuitwa wana wa
Mungu.
Ukisoma katika kitabu
cha Luka 6:19, Roho wa Uweza anapoingia ndani ya mtu unamfanya kuwa mtoto
wa Mungu. Roho wa uweza amegawanyika katika makundi manne ambayo ni Toba, Maombi, Maji na unafikia wakati wa kuchambua neno na kuhubiria
watu.
Roho wa uwezo (Wafilipi 4:13): Uukifika hatua hii anakuwezesha kufanya mambo yote. Wewe mwanamke kama kuna wakaka walikuwa wanakukataa na kukukimbia, sasa utaona wakaka wanajikanyaga wakitaka kukuoa. Kumbuka mwanamke ni zawadi na ndio maana mwanaume anakaa na kuomba mwanamke wa kumuoa.
Roho wa uwezo (Wafilipi 4:13): Uukifika hatua hii anakuwezesha kufanya mambo yote. Wewe mwanamke kama kuna wakaka walikuwa wanakukataa na kukukimbia, sasa utaona wakaka wanajikanyaga wakitaka kukuoa. Kumbuka mwanamke ni zawadi na ndio maana mwanaume anakaa na kuomba mwanamke wa kumuoa.
Mungu anaangalia wokovu wako, kwasababu Roho ya uweza ipo
ndani yako, usivuke nafasi ya Mungu kwa kufanya mambo yako bila ya kumtanguliza
Mungu. Mungu anasema pasipo yeye hakuna lililofanyika.
Roho wa Uweza kwa mtu wake anamsababisha mtu wa kuwa wa aina
Fulani, wanawake wengi wanalia kuwa Mungu amewasahau bure na hiyo sio kweli. Wakumbuke
kuwa wanahitaji kuwa na Roho wa Uweza ndani yao ili aweze kufungua milango
iliyofungwa na maadui zao.
Kila mtu anatakiwa kuwa na kitu Fulani ndani yake ambacho
kinafanya mtu afurahi. Ukiwa na Roho wa uweza ndani yako anakuganga mwenyewe na
kufanya miujiza. Unaweza ukashangaa unaomba na watu wanapokea miujiza yao
kwasababu Mungu amekukubali na umekuwa na kibali mbele za watu, kila jambo
ukifanya linapokelewa na kukubalika na jamii.
Ukisoma katika kitabu cha Zaburi 34:7, Malaika wa Bwana ni
Roho wa Uweza – ambaye ni muhimu maishani mwetu, na huangalia wamchao Bwana
kwanza ili kufanya maajabu yake. Mungu hubariki Yule amchae. Jitahidi kupende
kuwa na Roho wa ibada ndani yako na
kusababisha uweza utoke ndani yako. Kama ni mfanya biashara utaona wateja
wanamiminika kwasababu Mungu amekukubali
Mungu akiona ibada ipo ndani yako anafanya makao ndani yako
na hapo utaona mabadiliko katika maisha yako. Sasa unatakiwa kuona njia zako na
sio matendo.
Inawezekana kufanya mambo yasiyowezekana kama unakubali
kuacha dhambi na kumkubali Yesu. Uwe na mawazo ya kuwaza baadae yako na pia uwe
mwombaji mambo yako ya ubaadae wako na kwa kuwaleta watu kwa Yesu.
VITU VYA KUFANYA ILI
KUFANYA YASIYOWEZEKANA YAWEZEKANE:
i.
Ishi maisha matakatifu
ii.
Uwe mtu wa maombi
iii.
Walete watu kwa Yesu
iv.
Mungu anaruhusu maajabu yake
JITAHIDI KUWA MTU WA
IBADA ILI YAFUATAYO YATOKEE:
I.
Tabia ya mawazo ya dhambi inatoweka
II.
Roho wa ibada anaumbika kwako
III.
Roho wa uweza anakuwa ndani yako
Roho wa uweza anakupa wewe ujasiri, maana hakuna kitu
kitakacho kushinda na kusababisha kufikia mahali ambapo unataka kufika. Ondoa
uvivu, uongo, umbea bali tamani kumjua Mungu, Mungu anakubali wale
waliokubalika.
USHUHUDA: "BWANA wetu YESU KRISTO YU HAI"
APATA SIKU ZAKE ZA HEDHI BAADA YA KUKAA MIAKA MINNE.
Naitwa Magdalena, Napenda Kumshukuru MUNGU ilikuwa ni siku ya Jumamosi siku ya Uji hapa Kanisani, Mimi nilichaguliwa kwenda Kupika uji, baada ya kupika Uji na kunywa Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii akatoa Unabii akasema, Yeyote aliyekuwa na Ugonjwa unaishia Getini, na Akasema kuwa kuna mtu ambaye Hazioni siku zake yapata miaka minne sasa anakwenda kuziona, Mimi nililichukua lile neno kwani lilikuwa la kwangu.
Siku ya tarehe 17 nilipofika Nyumbani Usiku nilishangaa sana Niliziona siku zangu NILIFURAHI sana, NAMTUKUZA MUNGU kwa hili.
Pia nimeleta Zawadi za Shukrani kwa Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Mama Eliakunda Mwingira, Mchungaji David Mwakisole na Elibariki Urasa.
Namshukuru MUNGU kwa Kunipa Kibali KUSHUHUDIA kile Alichonitendea. Wewe ambaye bado Hujapokea Muujiza wako, USIKATE TAMAA, Mimi nilikuwa nakuja Ibadani kila Jumapili kwa Miaka minne lakini tarehe 17 ndiyo ilikuwa SIKU Yangu, na Wewe siku yako Ipo, Nenda kwenye UWEPO wa BWANA kila Wanapokusanyika Watakatifu, MARUFUKU Kukata Tamaa.
USHUHUDA: "BWANA wetu YESU KRISTO YU HAI"
MAGONJWA BASI,.....
Naitwa Wiston David namshukuru Mungu kwa neema ya Wokovu ambayo ninayo mimi, sababu kabla Sijaokoka nilikuwa nasumbuliwa na magonjwa ya kila mara, haipiti wiki mimi ninaumwa, ila baada ya kufika hapa Efatha na kufuata maagizo ya Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, ile hali imeondoka na tangu nilipo OKOKA mpaka leo yapata Miaka Mitano SIJAUGUA tena, Namshukuru MUNGU sana. Pia mimi nilikuwa mfanyabiashara ila kila nikipata Faida Pesa ilikuwa inanikimbia kabisa, ila baada ya kufika hapa EFATHA, sasa Biashara yangu inaenda vizuri na FAIDA Naiona.
Siku moja nilienda Kibaha kufanya kazi ya BWANA, na Mimi nilikuwa natamani kufungua Shule ya Nursery. Baada ya kufanya kazi ya BWANA nilipata mtu akanipa eneo na sasa nimefungua Shule yangu na inaendelea vizuri. Yamkini wewe unateseka na magonjwa njoo EFATHA Utapona maana kuna NGUVU ya MUNGU, mimi Nimemuona.