EFATHA MWENGE: NABII NA MTUME JOSEPHATE ELIAS MWINGIRA AHUBIRI SIKU YA JUMAPILI JUU YA "NAFASI YA UBABA"
Rumafrica iliweza kubahatika kuhudhuria ibada ya pili siku ya Jumapili 10/05/205 katika kanisa la EFATHA Mwenge jijini Dar es Salaam inayoanza saa 4 asubuhui mpaka saa 7 mchana. Ibada hii ilioongozwa na mwanzilishi wa kanisa la Efatha Nabii na Mtume Josephate Mwingira. Ibada hii ilikuwa ni ya toafauti sana na waumini waliweza kushangilia baada ya Nabii na Mtume Josephate Mwingira kupanda madhabahuni.
Nabii na Mtume Josephate Mwingiara
Katika ibada hii kuna mambo makuu kama matatu alilisisitiza na aliweza kuomba watu wanaopitia hayo aliyosisitiza kufika madhabahuni na kuwaombea wakiwa wamepiga magoti. Nisikumalizie uhondo huu ungana nami:
NABII NA MTUME JOSEPHATE MWINGIRA ALIOMBEA JUU YA
Nabii na Mtume Josephate Mwingiara
Katika ibada hii kuna mambo makuu kama matatu alilisisitiza na aliweza kuomba watu wanaopitia hayo aliyosisitiza kufika madhabahuni na kuwaombea wakiwa wamepiga magoti. Nisikumalizie uhondo huu ungana nami:
NABII NA MTUME JOSEPHATE MWINGIRA ALIOMBEA JUU YA
- - Waliofiwa na wanae baada ya kujifungua.
- - Waliofukuzwa na waume zao
IBADA ILIHUSU MAADA ILIYOMO KATIKA KITABU CHA MTEMBEO WA MUNGU.
Kitabu cha mtembeo ni kitabu kilichoandaliwa na Nabii na Mtume Josephate Mwingira ambacho kinakuongoza kwa muda wa mwaka mzima. Mtembeo na Mungu ndio maono aliyopewa Nabii na Mtume Josephate Mwingira juu ya kuwahamazisha waumini kutemembea na Mungu kila siku na baada ya hapo utapata mavuno siku yako ikifika.
TUNAONA KILE MUNGU ANATARAJIA WEWE KUFIKA
Vyovyote unavyofanya na kusogea hatua kwa hatua, ujue Mungu anakuhitaji. napofanikiwa au unapopitia magumu yoyote unatakiwa kubaki na Mungu na kufuata sheria zake. Mungu ameweka kitu ndani yako umtumikie. Ndugu zangu tusimsahau huyu Mungu wetu kwani kwani Mungu anakuhitaji na anamopango na wewe.
NAFASI YA UBABA
Mambo ya msingi ya kuzingatia katika maisha yetu, Mungu ametupa amri kumi lakini amri ya 2 na 1ni muhimu sana, amri hizi zinabeba manabii na torati.
Amri ya 1,2,3 zinamuhusu Mungu, 1-10 zimebebwa na neno zito “Mpende jirani yako”
Heshima ya ubaba unatupa kuwapenda wengine na kuwapokea wengine, amri ya nne inatupa kuishi nafasi ya ubaba, inatupa kufanikiwa duniani.
Nafasi ya umama ni kwaajili ya matumaini/ hizi lakini nafasi ya baba ni nafasi ya kuthibitisha, kukujenga kufanikiwa, imebeba mafanikio yako, ustawi wako.
Nafasi ya ubaba isipochukuwa nafasi kwako usitarajie kustawi, kama mzazi wako hatakutamkia ubaadae wako.
Asilimia kubwa watu wengi hawajatamkia ubaadae wa wanao na ndio maana maisha yanakuwa magumu.
Mungu anataka kufahamu nafasi ya ubaba na umuhimu, kuna wengine hawana wazazi au hawajui wazazi wao, au wengine hawajatamkiwa, kwa hiyo anayechukuwa nafasi yao ni baba yako wa KIROHO.
Mungu asipokuruhusu, hutaona ubaadaye wako ukichanua, kazi ya mbaraka ni kuruhusu jambo jipya kutokea katika maisha yako, kwa hiyo tafuta mpakwa mafuta akutamkie mbaraka.
Unapopata mbaraka wa ubaba hata kile kidogo kinaongezeka, nafasi ya ubaba wa Yule aliyekuzaa na akawa amekufa, na hakukuachia mbaraka, basi baba wa KIROHO anachukuwa nafasi hiyo.
Tunaweza kuwa na wahubiri wengi lakini tukawa hatuna wababa wengi, baba hutangaza ubaadae wa mtu aliyeshindwa kutatua tatizo lake lililomsumbua kwa muda mrefu.
Mungu anaheshimu nafasi ya ubaba katika maisha yako, ruhusu nafasi ya ubaba itokee kwako.
Unaporuhusu nafasi ikawa na mamlaka ya kutamka na ukaamini utakuwa mshindi. Ubaba kazi yake ni kuwezesha, kuamrisha jambo litendeke na kutokea. Ukirithia nafasi ya ubaba hutakuwa chini bali utakuwa juu sana na hutashindwa.
Na yeyote ambaye baba yake alimkataa, alimlaani, hawaelewani, alikufa kabla ya kupata ufahamu
Waumini wenye sida ya kufiwa na Baba yake, kuteswa, kugombana na baba zao na kufika hatua ya kulaaniwa na baba yake
IBADA YA KUTUNZA FEDHA ILIYOFANYIKA JUMATAUTU 15/05/32015
NAFASI YA UBABA
Comments