Rumafrica ilibata
kibali mbele za Mungu cha kuweza kufika katika kanisa la Nabii na Mtume
Josephate Mwingira la EFATHA lililoko Mwenge Dar es Salaam siku ya Jumapili ya
tarehe 19/07/2015. Ibada ya pili ilianza saa 4 asubuhi na kumalizika saa 7
mchana ambapo Nabii na Mtume Josepahte Mwingira aliweza kuwaomba wachungaji
wake watoe ujumbe wa Mungu kwa waumini na baadae aliweza kusimama na kuhubiri.
Sasa naomba nikushirikishe mamchache kutoka kwa watuminishi wa Mungu.
Picha ya Nabii na Mtume Josephate Mwingira katika ibada za nyuma
WANAOMNGOJEA BWANA
Hao wanaomngojea Bwana watatiwa nguvu mpya na wataruka juu
kama tai, mahali penye kupanda pana kushuka. Ukitaka kupanda unahitaji nguvu
mpya, anayeshuka ana nguvu ya kushuka, mfano Yusufu alikuwa haeshimiki na ndugu
zake lakini alikuwa na ndoto ya kuwa mtu wa juu, ndugu zake wakachukia kuwa
Yusufu kupatiwa ndoto.
Yusufu alipitia changamoto nyingi sana, lakini haikumpa
taabu kwani alijua yeye alioteshwa ndoto kuwa atakuwa juu, ndoto zako ulizonazo
zitatimia.
Kanisa la Yesu Kristo alitanyamaza kimya, Kanisa likinyamaza
basi Yesu amewakataa, nasi tunayemngojea Bwana tutapiga kelele na kumshukuru
Mungu. Safari yetu tuliyonayo haina kituo hapa duniani bali kituo chetu kipo
mbinguni basi.
HURUMA ZA MUNGU NA UPENDO WA MUNGU
Huu ni mwaka ulioamiwa kwa sababu huu ni mwaka wa kutembea
na Mungu, na Mungu ametuhurumia, Efatha ni kituo kilicho salama.
Yesu alikuja kwa sababu ya kukutoa kwa shetani na kukuweka
huru, tuliteswa na shetani na sasa tupo huru.
Zaburi 62: kwa sababu yetu sisi Bwana hatanyamaza,
atahakikisha unabarikiwa, wana Efatha tumepata neema ya pekee kwa hiyo
inatakiwa kuwaleta kwa Yesu ili waokoke. Mungu huko mbinguni hatulii kwa sababu
yetu ili uwe huru, tunaomba Mungu mbingu isinyamaze kwaajili yetu.
Shetani, wachawi waache wafanye yao lakini hawataweza kwani
neno la Mungu litatimia, tuachane na imani ya potofu ya kukatishana tamaa wana
Efatha, watu wamezoea kumtumikia Mungu asiye hai. Tunaposema Mungu wa Efatha,
tunamaanisha Mungu amesema nini na mbeba maono wa Efatha yaani Nabii na Mtume
Josephate Elias Mwingira.
Kama ulikuwa unashindwa kushuhudia, pokea nguvu ya
kushuhudia, tumepewa mamlaka ya matendo. Hutakiwi kuwa na mazoea ya kuzoea
huduma ya Mungu, unatakiwa kunyenyekea na kutii.
UPENDO WA MUNGU
Methali 8:17, nawapenda wale wanipendao na wale wanitafutao
kwa bidii wataniona, upendo ni nipe nikupe. Mungu atakupa yale unayoomba kama
kama unampenda na atakuzidhishia, tunampenda Mungu kwa imani, kama humuoni
Mungu basi unanafasi ya kuwapenda watumishi wake kwani hao wanatumiwa na Mungu
kuleta Baraka zako kwako na pia kuleta ujumbe kutoka Kwake
.
.
Mungu ni Mungu anayetuwazia mema, Mungu tunampenda kwa
kuwapenda watumishi wake kwani wao ni bomba lake la kupitisha ujumbe kwako.
Kama unasema nampenda Mungu wa Efatha na ukawa humpendi mbeba maono wa Efatha
basi wewe ni kichaa.
Upendo ni kumimina moyo wako kwa Mungu, Yohana 15:16 Sio
sisi tuliyemchagua Yesu bali yeye ndiye aliyetuchagua. Matunda yakikaa kwetu
basi tuombalo atatupa, Yesu ndiye aliyetutafuta na ndio maana leo hii unaenda
Kanisani. Unapofika Kanisani na kufurahia uwepo wa Mungu, unatakiwa kwenda
kuwatafuta watu wengine waje Kanisani na kumtumikia Mungu, unatakiwa kujiuliza
katika wokovu wako umeleta wangapi kwa Yesu.
Kumpenda Mungu ni kupeda yale mahusiano yake.
WEWE MTU WA MAANA
Marko 7:54. Kuna maneno sita yaliyotangulia kabla ya neno Efatha, lakini tuone haya matatu na mengine utasoma katika somo la MAANA hapo chini:
Marko 7:54. Kuna maneno sita yaliyotangulia kabla ya neno Efatha, lakini tuone haya matatu na mengine utasoma katika somo la MAANA hapo chini:
i.
Akazama juu mbinguni, alikuwa anatafuta Mungu
anamuonyeshe.
ii.
Akawaambia watu, watu wanakuja Kanisani kwa kile
tunachowaambia na sio tunavyowaona.
iii.
Efatha maana yake funguka, mambo yako yanaanza
kunyooka na kua mazuri.
Unapokuja Efatha unaona kila kitu kinakuwa cha maana,
unatakiwa kunyoosha maana yako na usiponyoosha maana yako, wengine watanyoosha
maana zao. Unachokifanya hakikisha maana yake inaonekana kila kitu unachofanya
lazima kiwe cha maana. Kama mwana Efatha kila kitu kiwe cha maana. Ukijua maana
unatoka gerezani na mambo yako yanaanza kuwa mazuri. Usifanye mchezo na mtu
anayejua maana ya Efatha. Ukifanya ujinga utaona moto wake. Watu wenye maana
hawarudi kwenye huzuni au ukame. Ukishaona umeanza kutengwa utambue umeshaanza
kupata maana yako. Kuanzia sasa anza kuwatenga Watu/Marafiki wasiokua na maana
katika maono yako. Chochote unachoona kinasababisha maana yako isitokee kemea
mapepo hao. Sii unakua wa maana hapa duniani tu, bali hadi mbinguni. Mtu hawezi
kuja kanisani bila ya kumtolea Mungu sadaka au zaka.
Ukiwa mtu wa maana unaenda kuamrisha adui zako. Mungu
anasema atawaweka chini ya miguu yako.
Mungu akiamua kukudharau anakudharau kweli, anakuweka chini
adui zako wanakwenda chini na anakwenda kuwaamrisha. Kuna watu wanakesha kwa
mabaya kwako.
Sisi ni viumbe vipya ambavyo vinafanya mambo makuu ya Kimungu
kwa watu wasiyoyapenda ya Mungu.
Kuanzia sasa:-
(i)
Vaa kwa maana
(ii)
Cheza kwa maana
(iii)
Toa sadaka kwa maana
Fanya
jambo lolote kwa maana.
Comments