MAHOJIANO SEHEMU YA PILI KATI YA WATOTO WA SHULE SALOME NA KEZIAH AMOS NDANI YA RUMAFRICA GOSPO ONLINE MAGAZINE
Kulia ni Keziah Amosi akifuatia mama yao Leah Amosi na Salome Amosi
BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KIDOGO KUSHOTO KAMA HALISOMEKI HAPO JUU
Rumafrica ilipata muda wa kuongea na waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania waishio Dar es Salaam aambao ni Salome na Keziah Amos . Waimbaji hao ni wanafunzi wa shule ya msingi na wanafanya vizuri sana katika ulimwengu wa muziki Afrika Mashariki. Watoto hawa wameachia DVD yao inayoenda kwa jina la AMETENDA. Sasa tuone sehemu ya pili ya maohojiano yaliyofanyika na Rumafrica
KABLA HUMJAANZA UIMBAJI MLISHAWAHI KWENDA STUDIO?
KEZIAH (Mkubwa): Namshukuru Mungu tulishawahi kuingia studio na mama yetu, kwasababu mama yetu anafanya karibu na studio ya muziki, kwahiyo kuna siku zingine tulikuwa tunaenda na mama yetu studio na kumuona anavyorekodiwa sauti yake. Tulikuwa tunashangaa sana kuona mama yetu akirekodiwa.
Kulia ni Keziah Amosi akifuatia mama yao Leah Amosi na Salome Amosi
SIKU YA KWANZA KUINGIA STUDIO KUREKODI NYIMBO ZENU MLIJISIKIAJE?
SALOME (Mdogo): Kwa kweli kwa mara ya kwanza kuingia studio kurekodi ni lazima uwe na mshangao nah ii ilitukumba. Kwanza sisi wenyewe haukutegemea kuwa tunaenda studio, mama yetu akatuita na kusema haya nendeni mkajiandae twende studio mkarekodi nyimbo zenu. Nakumbuka siku hiyo kila mtu alishangaa, tukawa tunamsumbua mama yetu atupeleke studio haraka.
KEZIAH (Mkubwa): Kiukweli nilijisikia vizuri. Nakumbuka siku hiyo nilihisi kitu ndani yangu, na nilipoambiwa tunaenda kurekodi binafsi sikuamini kwasababu kwanza tulikuwa tunajifunza, na tulikuwa bado hatujawa “fit” kuingia studio kurekodiwa. Lakini tunamshukuru Mungu tuliweza kufanikiwa kuimba na sasa tuna albam yetu.
NI MATATIZO GANI MLIKUMBANA NAYO WAKATI MNAREKODI AUDIO YENU?
SALOME (Mdogo): Namshukuruu Mungu tukuweza kupata matatizo yoyote, producer wetu hakuweza kuonyesha ukali kwetu.
UAMUZI WA MAMA KUWAFUNDISHA MUZIKI ULIKUWA UAMUZI MZURI?
KEZIAH (Mkubwa): Uamuzi wa wazazi wetu ulikuwa sio mbaya bali ni mzuri sana. Naweza kukutolea mfano, hivi leo hii nikiwa nimefeli mtihani wangu nitakuwa mgeni wa nani? Sina kazi, kila shule nikienda wananikatalia kwasababu nimefeli, hakuna kitu cha kunisaidia, lakini naamini kwa kufundishwa huku muziki kunaweza kunisaidia hapo baadae kumtumikia Mungu na nikawa nabarikiwa kifedha kwa kupitia uimbaji wangu.
UIMBAJI WAKO UNAFIKIRI UMEKUINUA KIIMANI?
SALOME (Mdogo): Nakumbuka mama alisema sina uhakika sana kama mnaweza kufanya vizuri nikiwapeleka kuimba sehemu nyingine, ni heri tukae tu pale kanisani kwetu aone uwezo wetu. Siku moja mama aliweza kutuunganisha na Mch. Katunzi na tukaenda kuimba, watu walitufurahia sana, na kuanzia hapo tukawa tunainuka “step by step” kihuduma na kiimani.
MAHOJIANO YANAENDELEA. NYIMBO ZAO ZIKO YOUTUBE NA MAHOJIANO HAYA YAO YAPO YOUTUBE, INGIA KWA KUTUMIA MAJINA YAO AU RUMAFRICA ONLINE TV AU RUMAFRICA
WAPIGIE: +255 714 494 974
Comments