Mwimbaji wa nyimbo za Injili na Mkurugenzi wa Sifa Foundation, Sifa John amemshukuru sana Mungu kwa kumuokoa katika ajali mbaya aliyopata akiwa kwenye gari yake. Ajali hii ilitokana na garia aina ya lori la mchanga kumgonga nyuma ya gari lake. Watu wengi walioona tukio hilo walidhani amekufa kutokana na mshindo mkubwa uliotokea.
Kwa kupitia facebook Sifa John amesema ni kwa neema ya Mungu na sio kitu kingine kwa kumuokoa katika ajali hiyo. Rumafrica inakupa pole dada Sifa John kwa hilo pitio ulilopata, ila zidi kumuamini Mungu kwani huyo ndiyo aliyekuleta hapa dunia na kukupa hilo gari lako. Anajua ulikotoka ulipo na uendako, zidi kumtumikia Mungu zaidi hapo ulipokuwa ukimtumikia.
Tunatambua Mungu amekupa mzigo mwingine wa kulea watoto wenye uhitaji, na akakupa kituo ambacho uliamua kukiita SIFA FOUNDATION ambacho kimefanyika baraka kwa watu wengi sana, na hasa hao watoto unaowalea.
Mungu azidi kukulinda na kukuinua katika kazi yako na huduma yako ya uimbaji. Mungu atakwenda kufanya mambo makubwa katika huduma yako, ataenda kukuinua na utasahau hata hili pitio ambalo unapitia. Tunakuomba uzidi kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji na pia kuwalea hawa watoto wenye uhitaji. Mungu azidi kukubariki in Jesus Name.
Comments