MCH. NOAH LUKUMAYI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" ASSEMBLIES OF GOD AHUBIRI JUU YA "UMECHAGULIWA KUWA SHUJAA"
Rumafrica ilibahatika kufika katika mkanisa la Mikocheni B
Assemblies of God (Mlima wa Moto) katika ibada ya Jumapili 30/08/2015 ambayo
ilianza saa 4 asubuhi. Katika ibada hii kulikuwa na kipindi cha shuhuda na pia
kuna baadhi ya washirika wa kanisa hili waliweza kutoa sadaka ya shukrani
kutokana na kufiwa na ndugu yao.
Mchungaji Msaidizi wa kanisa hili Mch. Noah Lukumayi aliweza kupata muda wa kuhubiri injili. Mchungaji alikuwa na haya ya kuhubiri.
Nakusalimu kwa Jina la Yesu Kristo. Leo hii tutazungumzia juu ya KUCHAGULIWA KUWA SHUJAA. Mashujaa ni watu wanaomtumaini Bwana na mara nyingi huogopwa na watu, mashujaa hawanung’uniki kwasababu wanafanya makubwa, mashujaa mara nyingi hawaogopi chochote bali wanamuangalia Mungu.
Unaweza kushangaa mbona mambo yako yanabadilika, mambo yako yanaanza kuwa mazuri, hapo tambua ya kuwa kuna malaika wamekuzunguka. Kila mtu anayesali katika kanisa hili la Mlima wa Moto atambue ya kuwa amechagua mahali sahihi na hautashindwa kwa jambo lolote.

Kuna watu watatamani kukusukuma lakini hautaanguka kwani
wewe ni shujaa wa BWANA. Mashujaa mara nyingi wamekuwa hawaheshimiki kwasababu
wana vita vya kipekee. Kuna maadui wengi sana wanawazunguka mashujaa ili
wawaangamize lakini wanashindwa.
Niongee na wewe ambaye hujazaa, Mungu yupo pamoja na wewe na
atakushindia. Ninaona Yehova akikushindia na kukutetea. Mapito unayopitia sasa
yanakwenda kutoweka kwa Jina la Yesu.
Hata kama unapitia magumuzii kumwamini Mungu wako kwani yupo
palepale na hajakuacha katika mapito yako. Kila jaribu lina mlango wake wa
kutokea, basi amini linakwenda kutokea.
Kuna watu wanakuona huna kitulakini BWANA anakuona wa thamani. Wengine wameweza hata kukudharau na kukutamkia maneno magumu kuharibu maisha lako, lakini nataka kukueleza kuwa BWANA yupo pamoja nawe, zidi kunyeyekea na kumuomba. Unaweza ukaonekana huna thamani lakini BWANA atakuchagua na kuleta mabadiliko mkwa kupitia kwako.

Kuna watu watakukatisha tama na kukuvunja moyo, wengine
watatamani udondoke lakini wewe simama na BWANA na usitishike wala kuogopa
kwani wewe ni shujaa. Kwa kila jambo unalofanya usitegemee akili zako wala
usiwategemee wanadamu kwani yupo Yehova
atakayekusaidia.
Ukiwa na BWANA, watu watafunga mlango wa mafanikio, lakini
utaona mlango huo huo unafunguka. Unachotakiwa kufanyaq ni kuwa mtu wa toba,
maombi na shukrani.
Watasema mengi lakini Bwana atakuinua zaidi ya hapo
Watasema mengi lakini Bwana atakuinua zaidi ya hapo
Comments