ASKOFU MH. DKT. GERTRUDE RWAKATARE AONGOZA IBADA KUU SIKU YA JUMAMOSI 24.10..2015 KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO ASSEMBLIES OF GOD
KUFUNULIWA MAMBO YAKO YALIYOZIKWA NA MAADUI ZAKO
Bwana Yesu asifiwe. Ni vizurii kuwepo nyumbani mwa Bwana, ni vizuri
kukutana na Mungu wako, ni vizuri kukutana na Baraka za Mungu.Askofu Mh. Dkt. Gertrude Rwakatare
Tunaona nchi ya Wafilisti ambayo ni nchi ya mashetani ilivyoweza kufukia visima vya Isaka ikidhani imemmaliza Isaka. Inawezekana kuna watu wamefukia vitu vyako hufanikiwi, lakini mimi ninasema siku ya leo vinaenda kufunuliwa kwa jina la Yesu na utaona maji yanabubujika.
Shetani ameshindwa kwa jina la Yesu, ninaona afya yako ikikurudia tena. Sio kila anayekuchekea anakupenda, unatakiwa kuangalia moyo wa mtu. Pia zidi kumtumikia Mungu na kufuata taratibu zake.
KWA MKONO WA MCHUNGAJI WAKO UNAFANIKIWA KWANI YUPO KATIKATI YAKO NA MUNGU
Soma Hosea 12:13 Kwa mkono wa Nabii Musa, Israel walitolewa Misri wakaingizwa Kanani, na kwa mkono wa Nabii, Israel walihifadhiwa. Kwa mkono wa Mchungaji mwamini anaibuliwa kutoka kwenye dhambi na anaingia kwenye wokovu, kwa mkono wa mchungaji mwamini anasimama na kustawi Kiroho, kwa mkono wa mtumishi wa Mungu mwamini anaokolewa kutoka duniani anaingia mbinguni kwenye uzima wa milele, kwa mkono wa mchungaji huyu mtumishi anaendelea mbele anakuwa na ushuhuda na anakuwa na ushindi, anakuwa ni muweza na anakanyaga dhambi na kazi za shetani.
Askofu Mh. Dkt. Gertrude Rwakatare
Leo hii nimesimama kama Askofu wako kati yako na Mungu, kati yako na shetani. Nimesimama katikati yako na magonjwa. Ninasema magonjwa hauna mamlaka juu huyu mtu kwani ni wa Yesu.
Ninasema ewe magonjwa utoke kwa jina la Yesu, magonjwa ya mifupa, majipu, ninasema magonjwa hamna mamlaka kwani nimesema kati yako magonjwa na huyu mwamini wangu. Nimesimama kati ya talaka, kukataliwa, kunyanyaswa. Ninasema talaka, dharau katika ndoa, mateso toka kwa jina la Yesu kwani huna mamlaka juu ya huyu mwamini. Mimi nimesimama kati yako na huu mlima unaozuia maendeleo yako, kushinda kwako.
Ninakutangazia wewe shetani hutakiwi kuwagusa watoto wa Mungu, kwani Mungu amesema usiwaguse masihi wangu wala msiwatende mabaya. Mungu alikemea nyoka jangwani ili watu wake wawe salama.
Askofu Mh. Dkt. Gertrude Rwakatare
Ninaongea na wewe muamini wangu kuwa kila siku simama na Bwana. Wenzetu zamani walikuwa na Nabii Musa aliyesima kati ya kifo na watu wa Mungu, kati ya vita na watu wa Mungu, kati ya magoonjwa na watu wa Mungu. Jangwani miaka 40 hakukuwa na dispensary au hosptali, hakuna aliyepasuliwa, hakuna aliyepewa kidogo, hakuna aliyechomwa sindano, ila Mungu alikuwa daktari wa madaktari.
Maadui zetu wanatumia mkono wa mtu lakini sisi tunatumia mkono wa Mungu kufanikisha mambo yetu.
USING’ANG’ANIE DHAMBI
Kuna wimbo huwa tunaimba unasema, “ Using’ang’anie dhambi itakupeleka pabaya” lakini kuna watu wameokoka bado wameng’ang’ania dhambi
Raheli alikuwa mke wa pili wa Yakobo mtoto wa Labani. Yakobo alipofikia wakati wa kuoa, baba yake alimwambia ukaoe huko nyumbani kwenu yaani kwa watoto wa mjomba wake dada yake na mama yake, wale walikuwa binamu zao, lakini kumbe Recho aliondoka na uchawi.
hata sasa kanisa la leo, wapo watu wameokoka lakini wamebeba vinyago vya kiburi wakiambiwa jambo wameshupaza shingo kama haiwezi kugeuka. Wapo watu wameokoka lakini ni wasengenyaji. Kama watumishi wa Mungu tunajitahidi kuwahubiria lakini wanasema hili Neno sio langu. Kama Askofu ninasema leo utubu kwa jina la Yesu, leo ondoa kila kile kilichokuwa chukizo mbele za Mungu kwa jina la Yesu
Tunakukaribisha
kanisa kwetu Mlima wa Moto Assemblies of God, lililopo jijini Dar es Salaam,
Mikocheni “B”. Ukifika Mwenge mataa waombe watu wa bajaji wakulete kanisa kwa
mama Gertrude Rwakatare. Siku ya
Jumapili kunakuwa na usafiri wa bure saa 2 asubuhi katika kituo cha Makumbusho
au Mwenge Mataa.
Tembelea
www.mountainoffiretanzania.blogspot.com au
www.rumaafrica.blogspot.com
Facebook kwa jina la Mountainoffire Tanzania.
Tembelea
www.mountainoffiretanzania.blogspot.com au
www.rumaafrica.blogspot.com
Facebook kwa jina la Mountainoffire Tanzania.
Comments