RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WATU WAZIDI KUOKOKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO ASSEMBLIES OF GOD SIKU YA JUMAMOSI 24.10.2015

Picha kwa hisani ya Rumafrica +255 715 851 523
Mchungaji Karisto Kyando aliweza kuwaombea watu walioamua kuokoka siku ya Jumamosi katika ibada Kuu iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God. Sababu kubwa ya ibada hii kufanyika Jumamosi inatokana na kushindwa kufanya Jumapili kwasababu ilikuwa ni siku ya Kitaifa ya kupira kura za kumchagua Rais wa Taifa la Tanzania pamoja na wabunge na madiwani. Mch Karisto Kyando aliwaombewa waokovu wapya kama ifuatatvyo, “Bwana anasema msijisumbue kwa jambo lolote na msiwe na wasiwasi, unachotakiwa ni kusali, kumuomba Mungu na kuwa mtu wa shukrani.

Mch. Karisto Kyando akiwaombea watu walioamua kuokoka

 Sasa naomba wewe uliyekuja kuokoka ufuatishe maneno haya, “ Sema, Ee Bwana Yesu, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi, asubuhi ya leo, ninakuomba Yesu ufute makosa yangu, ufute uovu wangu nilioufanya kwa kukusudia au bila kukusudia ninaomba unisamehe. Ninakuomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu, andika jina langu kwenye kitabu cha uzima. Kuanzkia leo ninamuamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yangu. Amen

Kwako wewe ambaye hujaokoka, tunakukaribisha kanisa kwetu Mlima wa Moto Assemblies of God, lililopo jijini Dar es Salaam, Mikocheni “B”. Ukifika Mwenge mataa waombe watu wa bajaji wakulete kanisa kwa mama Gertrude  Rwakatare. Siku ya Jumapili kunakuwa na usafiri wa bure saa 2 asubuhi katika kituo cha Makumbusho au Mwenge Mataa. Tembelea Facebook kwa jina la Mountainoffire Tanzania.




Askofu msaidizi wa kanisa la Mlima wa Moto Mch. Noah Lukumai









Comments