RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KUFANYA MKUTANO WA SIKU 8 ZA MUUJIZA GEZAULOLE KIGAMBONI-DAR

 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiongea na Rumafrica amesema kuanzia tarehe 21 hadi 28/02/2016 kutakuwa na mkutano wa Injili wa siku 8 za miujiza katika eneo la Gizani Gezaulole Kigamboni. Mkutano huo utaanza saa 9 alasiri hadi 12 jioni. Katika mkutano huo kutakuwa na zoezi la kufungua rasmi kanisa jipya la Mlima wa Moto lililopo Gizani Gezaulole Kigamboni. Mkutano huo utaambatana na maombezi kwa wakazi wa Kigamboni na watu wote ambao watafika katika mkutano huo. Akiongea kwa msisitizo amesema, "Watu waje kwa wingi sana kwa maana kutakuwa na mlipuko wa Injili na miujiza mengi itatokea katika mkutano huo", amejipanga na jopo la wachungaji kama vile mchungaji msaidizi wa kanisa hilo Mch. Noah Lukumy, Mch. Karisto Kyando, Mch. John Mianah kutoka Kenya na wengine wengi. Pia kutakuwa na waimbaji mbalimbali, baadhi yao ni Christopher Mwahangila, Happy Kwaya, Joybringers Kwaya, Manesa Sanga, Kasaki, Sifa Mkumbo na wengine wengi. Mwisho, ameomba watu waweze kufika bila ya kukosa.

Comments