CHAMUITA ARUSHA inamshukuru sana Mungu kwa kuweza kufanya tamasha kubwa ambalo limeweka historia kwa mwaka 2016 katika jiji la Arusha. Ilikuwa si rahisi ila kwa msaada wa Mungu tamasha liliweza kufanyika kwa mwitikio mkubwa sana, na kila aliyefika mahali hapo aliweza kubarikiwa kwa Neno na uimbaji kutoka kwa waimbaji waliochini ya CHAMUITA. Hakika tuliuona mkono wa Bwana ukitembea kwa watu wake.
Lengo la tamasha hili ni kutangaza CHAMUITA kwa wakazi wa Arusha na dunia nzima kwa kupitia mitandao na media mbalimbali. Katika tamasha hili kulikuwa na kwaya nne, vikundi vitatu vya Praise and Worship, madhehebu mbalimbali, maaskofu wawili, wachungaji saba.
Katika tamasha hili tuliweza kupata kondoo wapya waliamua kujiunga na chama hiki na wakaweza kuchukua fomu za kujisajili. Na hii inaonyesha ni namna gani Mungu wetu amekikubali chama hiki kuwa ni chombo chake cha kutumia kufikisha ujumbe kwa watu kupitia vinywa vya waimbaji.
Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kwa kanda ya Arusha kilizindiliwa rasmi 10.10.2015 katika kanisa la Maranatha Arusha. Mpaka dakikia hii kina wanachama wasiopungua 150. Rais wa Chama hiki kwa Tanzania nzima ni Nabii Mwanasheria Dr. Addo November na pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Tuone sasa matukio katika picha
Comments