Bibi Mzuri akiingia kwenye basi, akifuatiwa na Mama Joyce tayari kwa kuanza safari kuelekea Buza wakitokea Majohe kanisani.
Wakristo wa Kanisa Anglikana Mtakatifu Mathayo Majohe siku ya Jumatatu wamefanya ziara kwenye kituo cha watoto yatima, "Valentine Chidren's Home" kilichopo Buza, ambacho kinafadhiliwa na Askofu Dr Valentino Mokiwa wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam na wahisani kutoka nchi za nje.
Wakristo hao wa Majohe ambao waliongozwa na Padri Patrick Challo, walipata muda wa kuongea machache na yatima hao pamoja na uongozi wa kituo hicho. Ambapo pia waliwapa watoto hao zawadi za vinywaji baridi, nguo na fedha taslim shilingi laki tatu na themanini elfu (380,000)
Watoto wa kituo hicho wakiwa wameketi kwenye mkeka, pamoja na wakristo wa kanisa anglikana Majohe baada ya kuwasili.
Wakinamama wa UMAKI Majohe nao pia walishiriki ziara hiyo. Wa kwanza ni Mama Semainda, akifuatiwa na Bibi Mzuri.
Padri Meshack Malilo kushoto wa Mt. Benard Yombo Buza na Padri Challo wa Mt. Mathayo-Majohe wakiimba katika tukio hilo. Padri Malilo anjaiandaa kuchukua nafasi ya Padri Challo atakayeondoka tarehe 17 Aprili 2016 kuhamia Tabata Kisukuru.
Sala
Mlezi wa kituo hicho, Sister Ruth akieleza machache kuhusu kituo
Baadhi ya wakristo wa Majohe wakiwa wameketi pamoja na watoto yatima. Yote hii ni katika kutimiza maandiko.
Watoto wakiimba mbele ya wageni
Padri Challo akitoa neno
Mwenyekiti wa fellowship iliyoratibu ziara hii, Mama Mitti (aliyesimama) akizungumza machache
Bibi Mzuri akizungumza kwa niaba ya kikundi cha Umoja wa Akina Mama wa Kikristu (UMAKI) Majohe
Picha na taarifa kutoka Anglikana Majohe
Comments