USIKOSE IBADA YA MOTO WA KUTEKETEZA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KWA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE JUMAPILI HII
Baada ya kupokea baraka zako siku ya Jumapili ya Pasaka ya tarehe 27.03.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam, kama unavyoona picha hapo chini, sasa tunakukaribisha katika ibada ya MOTO WA KUTEKETEZA MAGONJWA NA SHIDA MBALIMBALI itakayofanyika ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 3 asubuhi ikiongozwa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
Ibada hii itakuwa ni ibada ya tofauti sana na ibada ulizowahi kuhudhuria katika kanisa lolote lile, hii ni ibada ambayo watumishi wa Mungu wakiongozwa na kiongozi wa kanisa hilo Dr. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare watakapomshambulia shetani anayekutesa kwa muda mrefu, kwa kufanya maombi ya moto na mazito ambao yatasababisha kuchoma maadui zako na kuteketeza kazi zao, utaenda kuteketeza magonjwa, laana, kutoolewa kwako au kuona, kizuizi katika maendeleo yako ya biashara, kuchukiwa, kuonewa, kudhurumuliwa, kesi mahakamani, kushindwa kupata wateja, pesa zako kupotea kwa matumizi yasiyo ya lazima, kutosoma Neno la Mungu, kutofunga na kuomba, majini yanayokutesa, ndoto chafu, kulogwa na wachawi, hamu ya kufanya ukahaba, kutopendwa na watu kazini kwako, roho ya kutokaa kazini kwa muda mrefu na mambo mengine kama hayo. Yule Mtenda Miujiza Yesu Kristo kwa kupitia watumishi wake atakwenda kukuokoa katika mapito hayo.
Tunamuona Mungu akifanya mambo mengi sana katika kanisa hili la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Watu wanakuja wakiwa na maisha magumu sana, lakini zidi wanavyozidi kuhudhuria ibada zetu na kujifunza kutoka kwa Mungu kupitia watumishi wake, watu hawa maisha yao yanaanza kubadilika na sasa ni watu ambao ukiwaona wanafanania na maisha ambayo Bwana wetu `yesu `kristo anatamani watu wake wayaishi.
KUOMBEANA WAKATI WA SHIDA NA RAHA
Katika ibada zetu tumekuwa tupo karibu sana na watu wakati wa shida na wakati wa raha. Unapoona mwenzako anashida furaha tumekuwa karibu sana kusaidia kimaombi na hata kifedha. na hii ni kutimiza lile agizo ambalo Bwana wetu Yesu Kristo alituachia la kupendana. Unapoona mwenzako analia na wewe yapasa kumsaidia huyu anayelia ili awe na furaha kama yako.
Tumeona kuna watu wanapitia matatizo mengi sana katika maisjha yao na inafika kipindi wengine wanakata tamaa ya maisha na kumkufuru Mungu, lakini kama kanisa linapoona hivyo huchukua hatua ya kuwa karibu na watu hawa na kuwafariji. Tunamashukuru Mungu watu wengi sana wenye shida kama hizo za kukata tamaa wameweza kubadilika na sasa ni waumini wazuri na wenye kuchapa kazi ya Bwana
Rose Rwakatare akimkumbatia mama yake Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
Mungu anawatumia kwa njia ya tofauti sana na wengi wanapokea mijujiza yao kupitia maombezi yanayoendeshwa hapa kanisani. Mlima wa Moto limekuwa ni miongoni mwa makanisa ambayo yanasifika sana katika masuala ya kufariji na kubalikwa kimwili na pia Kiroho. Ni kanisa ambalo limekubalika mbele za Mungu kwa miujiza na matendo makuu ya Mungu.
Watu wamekuwa wakiingia kanisani wakiwa na machungu moyoni lakini wakikaa na kusikiliza mahubiri ya watumishi ya Mungu, kuna nguvu za Mungu zinaanza kuwagusa na baadae wanajikuta wamefarijika na kuona ule uzito wa mzigo waliokuwa nao moyoni umetoweka.
KUSIFU NA KUABUDI
Kanisa hili limekuwa mstari wa mbele sana kuhakikisha wanajikita katika ibada ya kusifu na kuabudu. Ndani ya kusifu na kuabudu kuna siri kubwa sana mbele za Mungu. Kama Wakristo tunatambua ya kuwa Mungu wetu na Mungu wa kusifiwa na anapenda sana kuona viumbe vyake vinamsifu. Kanisa la Mlima wa Moto kwa kugundua hivyo likaamua kutimiza agizo hilo la Mungu la kumsifu Yeye.
Hata wewe unatamani kuona mtu akikusifu kwa mazuri, unapoona hivyo hakika moyo unakuwa mkunjufu na wenye amani. Sasa Jumapili hii tutamsifu Mungu wetu katika kanisa la Mlima wa Moto zaidi ya ibada ya Jumapili iliyopita 27.03.2016. Ninachokushauri kuanzia sasa anza kutenga muda kwaajili ya kumsifu Mungu wetu kwa kuimba na kucheza.
Katika kanisa la Mlima wa Moto, watoto wamekuwa mstari wa mbele sana katika zoezi zima la kumuimbia Mungu wetu kwasababu wanatambua umuhimu wa kusifu na kuabudu. Tunamshukuru sana Mungu kwani kwa kupitia sifa tumeona watu wakibarikiwa sana na wengine kufunguliwa katika vifungo vyao. Jumapili ya Pasaka watoto walipata muda mzuri sana wa kusherekea kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo kwa kumuimbia nyimbo ambazo ziliwakonga waumini wa kanisa la Mlima wa Moto pamoja na wageni waliofika katika ibada hiyo.
Jumapili hii ni zamu yako sasa ya kumsifu Mungu kwa kuungana na hawa watoto na baadae kutakuwa na maombi ya moto ya kumuangamiza shetani ambaye amekuwa akirudisha maendeleo ya mwanao katika masomo yake na katika kazi zake za kawaida.
Umejikuta unashindwa kupata ada ya shule au umejikuta mwanao anaanza tabia ya kuiga tabia mbaya kutoka kwenye watoto wenzake watukutu au mwanao amekuwa ni mtoto wa kushinda hospitalini kwa magonjwa au umekuta mwanao ni miongoni mwa wanaofeli darasani, lakini katika ibada ya Jumapili Mungu anakwennda kumteketeza huyu adui shetani kwa kazi zake chafu dhidi ya mwanao. Njoo kanisani ukiwa na imani ya kuwa haya yanakwenda kutendeka kwa Jina la Yesu Kristo
WAZEE WA KANISA MLIMA WA MOTO
Wazee wa kanisa na wainjilisti wa kanisa hili wamejipanga vizuri kwaajili ya ibada ya Jumapili kuhakikisha wewe unapona katika mapito unayopitia. Hawa ni wazee wenye upako kutoka kwa Mungu kwa kupitia Bishop wa kanisa hili Dr. Gertrude Rwakatare.
Watu wengi walipoguswa na mikono ya wazee hawa wameweza kupokea majibu yao na kufunguliwa katika mateso. Mikono yao ni mikono ambayo imeombewa na Bishop wa kanisa hili kwahiyo wanapokugusa kuna nguvu za Mungu unaanza kuzipokea kutoka kwa Mungu.
Mungu anawatumia wazee hawa wa kanisa kwa njia ya tofauti sana. Ndugu yangu usikose Jumapili hii kwani kuna jambo linaenda kufanyika katika nyumba yako kwa kutii agizo hili. Usiache kuja na ndugu yako au rafiki yako ili unapobarikiwa na wao wabarikiwe na wakawe mablozi mtaani kwako ya kwamba Mlima wa Moto kuna Munngu yule wa kweli.
IBADA NI KWA DINI ZOTE NA MAKABILA YOTE
Ibada za Mlima wa Moto ni za kwa dini zote, makabila yote na rangi zote. Tumeona watu kutoka katika dini zao wakimiminika katika kanisa la Mlima wa Moto na kutamani kujiunga na kanisa hili. Na wengine wamekuwa wakishuhudia jinsi Mungu alivyoongea nao na kuwaonyesha kanisa sahihi la kuabudu ambalo ni hili la Mlima wa Moto.
Tunatambua ni ngumu sana kuona mtu kutoka katika dini ambayo sio ya Kikristo na kuingia katika Ukristo, wapo wengi wametengwa na familia zao kwa kuhama dini zao. Kanisa la Mlima wa Moto limekuwa likiwapokea watu kama hao na kuwafundisha Neno la Mungu na wamekuwa wakibadilika taratibu na baadae wanakuja kuwa watumishi wa Mungu wakutegemewa.
Katika picha hapo juu ni dada ambaye alikuwa Mwislamu na sasa ameamua kuokoka. Kipindi anajiunga na kanisa hili alikuja akiwa na mapepo na mamjini yeye na familia yake. Siku ya Jumapili ya pasaka aliweza kutoa sadaka yake ya shukrani kwa Mungu kutokana na yae aliyoteb ndewa na Mungu tangia amejiunga na Ukristo.
Robert Mutta Rwakatare
Comments