Rais wa shirikisho la muziki nchini Addo Novemba akiongea katika usiku wa gospel hip hop
Rais wa shirikisho la muziki nchini Addo Novemba ameweka wazi dhamira yake ya kufanya kazi na wanaharakati waYesu Okoa Mitaa katika suala zima la kutokomeza mambo ya ushoga nchini Tanzania hususani kwenye shule za bweni na vyuoni.
Akiongea kama mgeni rasmi kwenye tamasha la Usiku wa gospel hip hop lililoandaliwa na Yesu Okoa Mitaa ijumaa ya juzi Addo alisema kuwa imekuwa kitu cha kawaida sasa kusikia habari kuhusiana na mambo ya ushoga kitu ambacho sio dalili nzuri kwa taifa.
Rais huyo pia alieleza kuwa tabia za aina hiyo kwa sasa zinapatikana zaidi kwenye shule hasa zile za bweni zenye jinsia moja na kwenye vyuo na kuahidi kushirikiana na wanaharakati wa muziki wa injili wa kufokafoka kutoka Yesu Okoa Mitaa ili kufikia sehemu hizo na kuharibu mazingira yote ya ushoga ambayo shetani ameyaweka.
Kwenye tamasha hilo pia Rais Addo alisisitiza zaidi umuhimu wa Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini na kisha kuwaombea watu waliohitaji kupokea nguvu za Roho Mtakatifu usiku huo.
Pichaa kwa hisani ya Milpa Media.