MCHUNGAJI WA KIROHO WA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE MCH. DK. NIKU KUTOKA ASHEREKEA MIAKA 50 YA HUDUMA YAKE YA UCHUNGAJI SIKU YA JUMAPILI 22.05.2016
MCH. NIKU ASHEREKEA MIAKA 50 YA HUDUMA YAKE YA UCHUNGAJI
Siku ya Jumapili 22.05.2016 Mch. Dk. Niku kutoka Marekani
alikuwa anatimiza miaka yake 50 ya hduma ya uchungaji. Sherehe hii ilifanyika
katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini dar es Salaam Tanzania kwa
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Mch. Dk. Niku ambaye ni Mchungaji wa Kiroho wa
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kusimulia historia yake kuanzia shule ya
msingi, safari zake za huduma ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kama Zambia,
Sweden na Marekani na sehemu zingine Mbalimbali duniani. Kanisa la Mlima wa
Moto Mikocheni “B” lilimuandalia keki na ua moja zuri sana, nay eye aliweza
kuwalisha wachungaji wa Mlima wa Moto Mikocheni “B” ikiwa ni ishara ya
kuwaambukiza upako wa Kihuduma.
Mch. Dk. Niku
Naye Mchungaji aliweza kumzawadia Bishop Dr.
Gertrude Rwakatare zawadi ya kitabu chake cha Jubilee ya miaka 50. Sasa naomba
usome ujumbe huu aliokuwa akiongea siku hiyo, alisema, “Bwana Yesu apewe
sifa..!!..Nakushukuru sana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwani umenipa surprise kubwa mno
uliyonifanyia ya kuniandalia keki. Mimi nilipokuwa ninawalisha keki nikaona
kweli kwa Yesu kuna utamu. Kuna kwaya moja ya Mlima wa Moto Mikocheni “B”
imeimba na kusema “Kumbukeni ulikotoka”
na mimi ninakumbuka nilikotoka.
Bahati Bukuku akaimba kuwa “Mimi
nimewazidi wote” na mimi ninasema “Nimewazidi wote” kwa miaka na kwa huduma,
lakini na nyie wote mmetuzid sisi. Hii ni “Personal statement”. Ni lazima
ujijue wewe ni nani na utambue kuwa wewe “Umewazidi wote”, uwe unakaa
Kigamboni, Temeke, Mbagala, wewe umewazidi wote. Ngoja nikuambie, Mungu
amenibadilishe niseme ushuhuda. Kuanzia, Primary School, kuja mikoche, kwenda
Kenya na Marekani.
Shule za zamani ilikuwa unaingia darasa la kwanza mpka la
nane ndipo unaingia shule za sekondari, kila mahali niliposoma shule na
nilipokwenda nilikuwa nampenda Yesu Kristo, nah ii nilipenda sio kwasababu ya
dini bali Yesu alikuwa rafiki yangu. Nilimpenda Yesu Kristo kwakuwa alinipenda
nikiwa na miaka 6, na nilijijua kuwa mimi ni mtoto wa Mungu .
Leo nikiwa kwenye
gari nilikuwa nasema, “Ukiwa mtoto wa Rais unafikiri utahangaika?”, huwezi
kuhangaika kwasababu wewe ni mtoto wa mtu mkubwa. Lakini na mimi ni mtoto wa
mtu mkubwa aliyeumba mbingu nan chi, na wewe ni mtoto mkubwa aliyeumba mbingu
na nchi .
Nilipokuwa naenda Nairobi, watu wakanambia unaenda Nairobi kwenye wahuni..!!!. Leo hii nashuhudia kuhusu huyu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, alikuwa mwembamba na usimuone leo hii yuko hivi kanenepa. Alikuwa ananambia wewe Mch. Niku mshamba, na siku zingine wananiita mke wa Yesu, au mama Superior. Na hawa walikuwa watatu, lakini leo Mungu amewababdilisha wanahubiri Injili. Ninachotaka kukutia moyo ni kwamba usijidharau wewe mwenyewe, hata kama mtu akikudharau lakini wewe usimdharau.
Mimi katika miaka ya 70 wakati wengine mlikuwa bado hamjazaliwa. Niliweza kutafuka kanisa la kuabudia nikapata kanisa la Baptist Church, na nilipofika hapo nikaanzisha kitu kinaitwa “Each One Rich One” ili kushuhudia watu ili niwa-inspire. Mimi maisha yangu ninayoishi ni kwaajili ya kuwa-isnspire watu ili watimize yale Mungu aliyoweka ndani mwao . Ninachojua ni kwamba kila mtu anahazina kubwa mno ndani ya moyo wake au mwili wake, kwani Mungu hajaumba mtu yeyote Yule ambaye ni “Failure” .
Kipindi hicho nilikuwa “Bold” na ile nguvu ya Mungu . Tumesikia leo katika ibada hii dada Safi Nyaule aliyekuwa mchawi akisema yeye alikuwa na nguvu za kichawi zilizomsaidia kutimiza mambo yake.” Na mimi ninasema Mungu akubariki.
Kwahiyo katika ile “Each OneRich One” nilikuwa nawashuhudia watu kumpenda Mungu. Wakati East Africa Railway wakati inataka kufungwa au kugawanywa, dada yangu akanambia nakuomba uangalie sasa ni kitu gani Mungu anataka kukifanya juu yah ii Railway. Dada yangu alikuwa ni mtu wa imani na ananipenda sana hata ndugu zangu mpaka sasa wananipenda sana na kuniheshimu sana. Dada yangu hata nikiwa nahubiri alikuwa anachukua nguo yangu na kwenda kuwawekea wagonjwa ili wapone, na Mungu kwa kupitia nguo zangu wengi walipona.

Kulikuwa na mtu wa West Africa alikuwa akitangaza kuwa kuna
kazi zinapatika, nilisafiri kutoka Nairobi kuja Tanzania kupata “Interview”
iliyokuwa inafanyika Africana Hotel, wakati tunakwenda kwenye interview na
tulipofika huyo baba akasema kwani tutamlipaje?, nikasema mimi mtoto wa
Mwakasege kwqsababu natafuta kazi nilimpe tena, nikasema “No Sense”, nikiwa
nimekasilika nikasema, “My God has Created nchi yote” na huyu baba anafikiri
yeye ndiye anaye-control? Katika interview yetu kulikuwa na wazungu watatu,
mmoja alikuwa USAID akaniuliza “You speak English” nakamwambia “Yes” akasema
tutakupa kazi USAID, nikashukuru sana.
Nikaenda Nairobi nikafunga mizigo,
nikarudi sikwenda USAID nikaingia ubalozi wa Marekani. Kipindi hicho nikawa
sifahamu USAID ni ipi? Mimi nikawa naomba Mungu kuniongoza ila ninachojua ni
Mungu tu. Nikaenda “USA Embassy” ambayo zamani ilikuwa ni “Nationa Bank” kwenye
ghorofa ya nne.
Siku moja nikakutana na wale waliotaka kunipa kazi USAID pale “USA
Embassy” wakaniuliza, wewe sio ndio tulitaka kukupa kazi USAID? Nikawaambia
mimi nilikuwa sijui nikajua wote ni wamoja. Wakanaambia wewe kaa hapa. Kuanzia
pale nikawa namshuhudia Yesu Kristo nikaanza kwenda Temeke wakati kipindi hicho
Ilala haikuwepo.
Sisi na mchungaji Taitus kutoka ubalozini tukasema tunakwenda
kujenga kanisa ambalo leo ni kanisa la Ilala, tulikuwa tunasema pesa yote
inayotoka ubalozini inakwenda kujenga kanisa. Nikasema kuanzia sasa nitakuwa
nazunguka kila mahali nikimhubiri Yesu Kristo hata kama watu walianza kutucheka akiwemo mama
Rwakatare.
Siku moja nikakutana na mama Rwakatare akiwa ameokoka na
kujazwa Roho Mtakatifu nikasema maombi hayarudi bure. Bishop Dr. Gertrude
Rwakatare aliweza kuandaa mkutano mkubwa sana pale UHURU jijini Dar es Salaam,
tuliona miujiza ya vipofu kuona, kulikuwa na katoto kadogo kana. Kipindi hicho
nilikuwa kijana nikihubiri huyu Yesu.
Mimi huko Marekanini ni m-missionary wa kuwatafuta watu wasisahau kwao, kuyahamasisha mataifa yasimsahau Mungu. Mimi nimemaliza hapa hapa Dar es Salaam. Nakumbuka tulikuwa tunahangaika sana tukizunguka kuhubiri Injili watu waokoke. Kwasasa nimemaliaza hapa Dar es Salaam kuhubiri nab ado naendelea kuzunguka duniani kuhubiri Injili.

Tuliweza
kufika Kimara katika kanisa la Kimara Assemblies of God lililopo jijini Dar es
Salaam kushuhudia, niliweza kushuhudia na kuhubiri, lengo langu sio kuwa na
kanisa ila kupanda wachungaji waitwe wachungaji. Ukiitwa kuwa Engineer uwe
Engineer, kama ni Mwalimu uwe Mwalimu, kama ni mwanasiasa uwe mwanasiasa lakini
mwanasiasa wa Yesu.
Nikiwa hapa hapa Tanzania nikawa najitahidi kuzunguka
kuhubiri na kujitoa kwa kila kitu nilichonancho, marta nikasikia sauti ya Mungu
kuwa unatakiwa kwenda kuhubiri, nikauliza, “Mbona nahubiri kila mahali kama
vile Kenya, Uganda?” Mungu akanambia, “Sasahivi utakwenda Sweden”, tukiwa
tumetoka kushuhudia Kibaha na mch. Bundi katika kanisa la Kiluteli, nikiwa
kasichana kazuri, nilikuwa napenda kuvaa vizuri hata watu kutoka American
Embassy wakitaka kuvaa nguo za Kiafrika walikuwa wanakuja kwangu.
Nakumbuka nilikuwa na nyumba yangu Magomeni mapipa na kipindi hicho kulikuwa hakuna nyumba nyingi ila kulikuwa na nyumba moja nzuri ya kigae, watu walikuwa wanajaa, watu walikuwa wanapenda kuja kwangu, nilikuwa napenda sana kuwaalika kuja nyumbani kwangu, nilikuwa “Hospitable” Kwa kukaa na Yesu Hizo zote ni kalama za Mungu, na mapenzi ya Mungu.
Baadae niliamu kuhama na kwenda Mikocheni Branding Cinema,
huko nikawa na vyumba vingi. Nikamshukur9u sana Mungu na hiyo yote ni kwasababu
ya kumtumikia Mungu na kumshukuri
kumshukuru Mungu. Mungu alianza kutenda miujiza hapa Tanzania, na
hukonkusunguka kote duniani hakukuanzia Marekani bali kulianzia hapa hapa
Tanzania.
Na kulikuwa hakuna watu wa kunisaidia ila alikuwepo Mungu Baba. Kama
wewe ni mtoto wa Mungu unatakiwa kumtumikia kwa asilimia 100, usiwe mtu wa kuja
Jumapili na ukitoka kanisani hakuna unachofanya kwa kazi ya Mungu.
Mimi “I Walked, I Talked, I think Jesus Christ, nimuinuaje. Watu wampende Yesu. Nikiwa Kibaha nahubiri wakati nahubiri watoto wa shule waliweka ramani ya Scandinavia. Unajua unapohubiri “sometimes” Mungu anakupa mambo Bwana akanambia, “Niondoke Tanzania mnamo July 1977 niende Ulaya”. Nikasema, mimi msichana naenda Ulaya kufanya nini?

Unajua muongo anamfuata mwanaume, na huyo
mwanaume ujue hamjui Yesu Kristo. Hakuna aliyeelewa ila babu na ndugu zangu wa
“family”. Dada yangu akanambia kama Mungu amekutuma wewe nenda tu, nikasema,
“Kwasababu Mungu amesema nitatii” Nikaondoka Tanzania nikiwa sina hata senti
kumi ila nikamuomba Mungu akanipa nauli.
Nikaelekea Nairobi kuwaaga ndugu zangu
na rafiki zangu, baada ya hapo niende Itali nikamuaga dada yangu kwasababu
katika akili yangu nilijua ninaenda kufa tu. Kuna mwimbaji Bahati Bukuku leo
katika ibada hii ameimba amesema, “Mbeba maono hafi”.
Nakumbuka kwa mara ya
kwanza kumuona Bahati Bukuku ni kipindi kile ambacho alitoa albamu yake ya
kwanza akiwa amevaa kilemba kikubwa kichwani na akiwa mwembamba sana. Nakumbuka
nilitamka maneno kuhusu huduma yake na kusema, “HUYU ataimba na atarudi nyuma.
Na leo nimesikia kutoka kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuwa hajarudi nyuma.
Niliwasiliana na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuwa nataka nije Tanzania katika kusherekea miaka yangu 50 ya huduma, niwaambie watu kuwa “INAWEZEKANA” usirude nyuma, usi-compromise inawezekana kwasabau Mungu wetu ni mkubwa, ni shetani gani atakayenishinda kwa kuwa Mungu alisema shetani yuko chini ya miguu yako.

That is what I was talking na kufikiria na ndio maana nimeweza kusimama kwa
kuwa katika mawazo yangu, namuona Mungu ni mkubwa kwangu, sikupata vishawishi.
Kulikuwa na watu wengine walinitegea ili wanikabe ili waniharibu, ila kwa kuwa
Mungu alikuwa upande wangu akatuma malaika wake wakashindwa kunikaba.
Siku moja nilitoka kusali katika ile sala ya usiki Ilala
kanisani hapa jijini Dar es Salaam na kesho yake nikawa na safari ya kwenda
Uganda kushuhudia nikasema sasa ngoja nikatishe jangwani ili nifike nyumbani
kwangu Magomeni. Wakati nimeacha watu wakiendelea na maombi kanisani. Wakati
nakatisha jangwani huku naimba na nimejaa Roho Mtakkatifu, wanaume wawili nyuma
yangu wakaniuliza wewe nani?
Mch. Dr. Niku kutoka Marekani akimkabidhi kitabu chake cha miaka 50 ya Jubilee katika huduma yake ya uchungaji.
Nikajiambia hawa ni walewale Malaya, wakaniambia
nisimame, na mimi nikagoma kusimama wala kuangalia nyuma, wakati huo huo
kimwili naogopa na nywele zimesimama kwaajili ya hofu. Nikaanza kuongea na
Mungu na kusema, “Mungu mimi sitasimama kwasababu unajua nimetoka wapi na
unajua kesho nasafiri ninakwenda Uganda” Wanaume hao wakanambia, “Unalinga
sio?” Mbele yangu kulikuwa na majani marefu na kamto kama maji. Wanaume hao
wakanambia ukifika hapo tutakukaba kwasabau hapo kuna kagiza.
Nilipofika katika kale kamto kulikuwa
hakuna daraja ila kumweka majiwe kwaajili ya kuvukia, nikakanyaga jiwe la
kwanza na la pili, ghafla mbele yangu nikaona mtu mwanaume amevaa kanzu nyeupe
anakuja, na alipokaribia kwangu na mimi nikageuza safari ya kwenda nyumbani
nikawa namfuata huyo mtu na mbele yetu kulikuwa na makaburi.
Tulipofika kwenye
taa Yule mtu akapotea ghafla na hapo kulikuwa na makaburi. Nilichokifikiria
akili nilijua ni jinni. Nikaona ni heri nilirudi kwa wale waliokuwa wanataka
kunikaba kuliko kwa huyu mwanaume aliyepotea ghafla. Nikiwa sijielewi vizuri nikaondoka katika
eneo hilo na ghaflla nikaona niko nyumbani kwangu bila kujijua.
Nilipoingia nyumbani kwangu nikawa bado na ule woga na fahamu zangu hazijawa sawa, dada yangu akataka kujua nini kilichonitokea, nikamueleza yote, naye akaniambia, “Dada siumeokoka?, Mungu alikutumia malaika wakuokoe. Nikajiambia kuwa Yule hakuwa malaika ila alikuwa Yesu mwenyewe.

Ninachotaka kusema ni kwamba, majaribu ni mengi na
nimeyapitia mengi, lakini ninamshukuru Mungu kwakuwa amenilinda. Nikaondoka
Sweden nikawa bado ninamuomba Mungu anisaidie ninunue magitaa kwaajili
wanakwaya, nipate pesa kwaajili ya kusaidia makanisa. Bado ninamuomba Mungu.
Katika kitabu change nimeandika MIUJIZA BILA KUONA.
Nikiwa Sweden nikaenda
katika ubalozi wa Tanzania na kuwaambia mimi ni Mtanzania nimekuja kuhubiri
Injili, wakanicheka sana, wakashangaa kwasabau wengine wanaenda huko kutafuta
kazi halafu mimi nimeenda kuhubiri. Nikawaomba wanisaidie kutafuta kazi ya
kujishikiza kwasababu lengo langu lilikuwa kuhubiri Injili na ninaishi kwa IMANI,
ila nahitaji kupata pesa ninunue magitaa ya kanisani, wakaniuliza, “Wewe una
familia?”, nikawajibu “ndio” .
Lakini akili yangu ilikuwa kusaidia watu wa
Mungu kundelea kumtukuza Mungu. Nikiwa hapo Ubalozini wakanambia kuna kazi
lakini wanahitaji mtu anayejua Kiingereza, Kiswidishi na Kifaransa, nikawaambia
“Ok sawa”. Nikajiambia moyoni hajilishi wanataka watu hao ila mimi ninachojua
ni kazi yangu, na pesa nitakazopata si kwaajili yangu ni kwaajili ya kazi yako
Mungu. Baada ya hapo wakanambia “Njoo uje kufanya kazi” Nikaanza kufanya kazi
pale Ubalozi, lakini ikawa bado, kwani nilikuwa nahitaji kurudi Tanzania.
Nikiwa nimerudi kutoa Sweden, mimi na wanawake wengine akiwemo Bishop Dr. Gertrude Rwakatare tukafanya mkutano katika ukumbi wa Lumumba Hall hapa jijini Dar es Salaam. Akaja mama Sofia Kawawa, kwahiyo tulikuwa tunasghulika na wakuu wa siasa na ukumbuke tulikuwa bado tunajishughulisha na siasa. Hata kama mimi nilizaliwa kijijini kwenye kajumba na maji kuyapata ni mpaka uende mile nyingi, lakini nilijua ninachokifanya ni kwaajili ya MUNGU.

Ninachotaka kukuambia ni kwamaba Mungu anapokubariki mtolee
sadaka ya shukrani kwani atakubariki zaidi
Wakati nahubiri katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam
nikijianda kwenda Mwanza kuhubiri, kuna vijana wawili wataka niende Zambia
kuhubiri nikawaambia haitawezekana kwasababu naenda Mwanza. Wakati naenda
kukata tiketi katika kituo cha Railway karibu na headquarter ya Police hapa Dar
es Salaam, Mungu akanambia huendi Mwanza unaenda Zambia. Nikajiuliza mbona hawa
watu siwafahamu?
JE, UNGEPENDA KUJUA KAMA ALIENDA ZAMBIA NA KILIFANYIKA NINI HUKO
JE, UNGEPENDA KUJUA KAMA ALIENDA ZAMBIA NA KILIFANYIKA NINI HUKO
JE, UNGEPENDA KUJUA SAFARI YAKE YA SWEDENI NA MIKASA GANI
ILIMKUMBA
JE, INGEPENDA KUJUA SABABU GANI ILIMFANYA ATOKE SWEDEN NA
KWENDA MAREKANI?
JE, UNATAKA KUJUA KITU GANI KILIMSABABISHIA YEYE KUTAKA
KUJIUA NA NI NANI ALIMUOKOA?
JE, MALENGO YAKE NI YAPI MPAKA SASA KATIKA HUDUMA YAKE?
USHAURI GANI AMEUTOA KWETU SISI?
JE, MALENGO YAKE NI YAPI MPAKA SASA KATIKA HUDUMA YAKE?
USHAURI GANI AMEUTOA KWETU SISI?
BASI TEMBELEA: Youtube kwa jina la Mlima wa Moto au Rulea
Sanga au tembelea blogu yetu www.mountainoffire .blogspot.com angalia Video au
ingia Facebook kwa jina la Mountainoffire Tanzania
MUNGU AKUBARIKI SANA
MUNGU AKUBARIKI SANA