SHUHUDA KUTOKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI 22.05.2016: APONA AJALI YA GARI WANAE WAWILI WAOLEWA ANUNUA KIWANJA
Siku ya Jumapili 22.05.2016 katika ibada ya UKOMBOZI katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini Dar es Salaam, muumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” alikuwa na haya ya kushuhudia na kumshukuru Mungu, “Bwana Yesu apewe sifa. Tunashukrani ya pekee kabisa kusimama mbele ya madhabahu hii ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” tukimshukuru Mungu kwaajili ya mama yetu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kutuombea masaa 24. Tulikuwa tunatamani sana kuja kushuhudia lakini hatukuweza. Tulipata neema ya mtoto wetu mpendwa kufunga harusi kupitia madhabahu hii, tunamshukuru Mungu kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kuweza kutusaidia, kwa maana siku hiyo kulikuwa na mambo hayajakamilika sana na yeye akanambia nimuone Muhasibu wa kanisa mama Martha na akaweza kutusaidia kiasi fulani cha pesa. Harusi yetu ilienda vizuri sana. Mwezi wa 9/2015 tukiwa tunatoka Moshi tulipofika karibu na Wami, gari tuliotoka nayo Rombo ilichomoka tairi la kushoto, kwa kupitia maombi ya Bishop Dr. Gertrude Rwakatare basi zima tuliweza kupona.
Lingine ambalo Bwana alitutendea baada ya kupata baraka katika madhabahu hii ni juu ya mtoto wetu mwingine ambaye na yeye ameolewa. Baada ya kuolewa 7/4/2016 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alituma wawakilishi kama Mch. Noah Lukumay na mke wake, Mch. Nnko na Mch. Francis Machichi. Katika ibada iliyofanyika katika kanisa la Maaskofu Kurasini jijini Dar es Salaam, Mch. Noah Lukumay aliweza kufanya maombi na watu waliokuwepo mahali pale waliweza kuguswa na maombi hayo na ile sherehe ikabadilika kuwa ibada. Nwashukuru sana wachungaji wa kanisa hili na waumini wote kwa maombi yenu. Tunamshukuru Mungu pia tumekuwa waaminifu sana kumtolea Mungu fungu la kumia, hata tukipata 5,000 tunamtolea Mungu. Tulipomtolea Mungu fungu la kumi siku ya kwanza, Mungu akaweza kutuelekeza sehemu ya kwenda kununua kiwanja. Tumekuwa tukipata muelekezo wa Mungu kupitia fungu la kumi. Pia tumekuwa tukifuatilia sana mahubiri ya Bishop wetu na kila kitu anachotuambia tufanye kwa mfano kupata mafuta ya upako, kalam za upako, kuleta fungu. Hivyo vyote vimeleta majibu maishani mwetu. Asanteni