RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DANSTAN MABOYA ALIVYOZINDUA RASMI SEMINA YA MID-CROSSOVER KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


Siku ya Jumapili ya 26.06.2016 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa na ujumbe mzito katika ibada ya kufungua rasmi semina ya CROSSOVER ambayo ilifunguliwa rasmi na Bishop Danstan Maboya. Semina hii inaendelea mpaka Jumapili ya wiki hii hapa Mlima wa Moto kuanzia saa 9 mchana hadi usiku. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa na haya ya kusema “Bwana Yesu Apewe Sifa!!. Jamani Majaribu ni mengi, na majribu ni kama maji ya moto hayaunguzi nyumba na katika jaribu kuna mlango wa kutokea. Hata mambo yakiwa mabaya acha kuzila kanisa. Wengine wanafikiria kuwa Mungu wao amewaacha, nataka kukuambia kuwa Mungu wako hajakuacha.

Ukisoma Nahumu 1:9 Neno la Mungu linasema, “Unawaza Nini Juu ya Bwana?” Katika mapito yako unawaza nini juu ya Bwana? Bwana atakomesha majuto na misukosuko yote. Kwahiyo ukijua kuna Bwana pembeni yako hata ukipita kwenye jaribu la namna gani utapita tu. Ukisoma katika kitabu cha Kutoka 3:6-8, unatakiwa kutafakari kama sisi ni wanadamu na tupo duniani na kwamba tunapatikana na mamabya na tunapatikana na mema na tunapatikana na mazuri.

Unapomaliza nusu mwaka unatakiwa uwe na sababu ya kutafakari uwepo wa Mungu katika maisha yako, lakini pia uwe na akili ya kuwaza kwamba nusu mwaka nitaanzaje? Na ndio maana semina hii tumeweka ili tuweze kumkabidhi Mungu ilia pate kuwa pamoja nasi ili yale mabaya ya nyuma yasitupate tena lakini mema yaendelee kuimalika na yakupate kwa jina la Yesu.

Katika mwaka huu 2016 tumeanza na kishindo na vilio vya hapa na pale, watu wengi wamekuwa wakilia, wengine wakilia na magonjwa, pesa, biashara haziendi, kwa kweli kwa macho ya kwaida watu wana vilio hata kama watu hawasemi, na wengine walikuwa na uwezo sana zamani lakini leo wamekwama na wanatamani kuwa na Mungu. Wengine wanadaiwa na ukiwadai wanasema, “Usiwe na wasiwasi tu nitakulipa”. Kwakweli wapo watu wengine wamenasa

Nataka kuongea na Roho yako ya ndani ya mtu ambaye amenasa na anashindwa kuendelea. Ulikuwa na maisha mazuri, lakini umejikuta uko mahali unashindwa kuendelea na mahali ulipo hauna raha. Ile rajha ya mara ya kwanza imepungua.


Sitaki uingie na uchungu nusu mwaka kuanzia Julai mpaka Desemba 2016. Nataka uingie na furaha, nataka uingie na matumaini, nataka uingie na Mungu, akushike kwa mkono wa kuume wa haki Yake. Bwana Yesu apewe sifa.

Wako watu wamekwama na madeni, niangalie sana na sura za huruma. Kama huna deni la benki basi unalo la SACCOSS au la PRIDE au la MPEMBA nyumbani kwako. Ninaongea na wewe mwenye madeni ya kwamba fedha na dhahabu ni mali ya Baba yako Mungu, hata kama una deoni kubwa la namna gani, Mungu anao uwezo wa kukulipia, uwezo wa kukunansua. Nataka mwezi Julai usikufikia ukiwa na masikitiko na machungu. Bwana anasema nimesikia kilio chako, nimeona madhaifu yako.

Unajua kungekuwa na mahema ya kuweka nyumbani mwa kila mtu, basi magari yasingepita, kwa maana kila nyumba kuna msiba, huzuni. Watu wengi wana mahema na wameweka mioyoni mwao, na leo ni siku ya kularua mahema na matanga, mateso, huzuni, misukosuko. Yaani ukifungua mioyo utatatua kukimbia kutokana na machungu yaliyo ndani mwao.

Siku moja kulikuwa na mkutano wa akina mama Dodoma (WWA) na mchungaji Maboya katika kanisa la Mch. Mhina, tukawa tumekusanyika tunaomba, “Mungu tunataka tukuone, Mungu shuka” Mtu mmoja akasema nimemuona Malaika, watu tukakimbia mbio, nikajiuliza Je, angeshuka Mungu ingekuwaje? Ninaomba Mungu ajivunue kwako, Mungu ajivunue kwa matendo makuu katika maisha yako.

Mama mmoja nyumba yake ilikuwa inauzwa kwani deni lake ni kubwa. Watu wakaanza kusogelea katika ile nyumba ili wanunue. Mungu ataabisha maadui zako kwa jina la Yesu, Mungu atafanya njia pasipo na njia kwa Jina la Yesu.

Bishop Danstan Maboya siku ya Jumapili 26.06.2016 aliweza kuzindua rasmi semina ya Mid-Crossover Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Semina hii ambayo itahitimishwa Jumapili hii na siku ya Ijumaa 01.07.2016 kutakuwa na mkesha mkubwa sana Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwaajili kuiombea miezi sita ijayo kumaliza mwaka. Na hivi ndivyo alivyonena, “Ninamshukuru sana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa ujumbe wake wa SIKU NANE MUNGU AKAGUE MAISHA YAKO. Sio kila mtu anweza kuwaza hili, kwani watu wengi sana hatuwezi kukagua maisha yetu. Hata kwenye nyumba zetu panya akiingia kwenye nyumba ndipo watu wanaanza kujiuliza, “huyu Panya kaingilia wapi?” Lakini kwa watu wenye kukagua nyumba zao, panya hawezi kuingia.

Mungu hakuingiza mwaka huu kwa bahati mbaya, na yoote tyaliyokuwa yakitokea hayakutokea kwa bahati mbaya. Yeye mpango mkubwa anataka uwe na akili yaani fikra zako lazima zifanyiwe mabadiliko. Unatakiwa kuangalia hatua na hatu ya kuendea. Na la kwanza lazima ufanya mtiririko wa KIFALME. 
Biblia inasema waaminini Manabii mtafanikiwa, na Mungu anasema kondoo husikia sauti ya mchungaji. Nabii umwamini tu lakini unakauka, ila wa kuongea naye ni mchungaji. Ndipo tatizo linapokwenda kutoke pale unapokwenda kuchukua Nabii kuwa Mchungaji na Mchungaji kumfanya kuwa shemasi, lazima utapa homa ya Kiroho. 
Kondoo huisikia sauti ya Mchungaji, kwahiyo sisi “Antena” zetu lazima tuzitengeneze kwa maana Manabii wanatakiwa wasikilize halafu wachungaji waweze kuchuja kama Unabii ni feki au “original”. Unatakiwa ukipewa unabii na Nabii unamuuliza mchungaji kuwa kuna ujumbe nimepata kutoka kwa Nabii, Je, Huu ujumbe ni feko au “original”, na mchungaji wako atakuambia kama ni “original” au feki, basi hapo mtakwenda pamoja. Lakini watu wengi tunakabiliwa na haya kwasababu wengi wenu sio kondoo ni mbuzi.

Sasa kumshilikisha mchungaji inakuwa ni dhambi au ni uhaini Fulani, kwa maana utasikia Nabii anakuambia haya maombi nayokuombea usipeleke popote nataka kuku-“surprise”. Ninakuambia kwa kweli nabii huyo ataku-“surprise”!! . Kwasabau mwanafunzi humshilikisha kwa mkufunzi wake na hili ndio eneo ambalo inatokea shida.

Kama Bishop Maboya, kwa uzoefu wangu mdogo nimekuja kuona katika watu kumi walioumizwa basis aba wameumizwa na Manabii na hawajaulizwa na wachungaji. Kwasabau utakuta hata zile kanuni za Kifalme, unatakiwa kutowaogopa manabii, lakini ukiwa na mchungaji huwezi kuongea ila mnaweza kubishana na kupata muafaka bila kuogopana. Ukimfuata mchungaji wako lazima utaona upendo na mpenyo, na hiyo itakusaidia kujua Uchina au Uingereza.

Sasa katika kipande hiki cha miezi sita ijayo kuanzia Julai mpaka Desemba 2016, kama utasikiliza sauti utafanya vyema. Na sauti hiyo siyo ya kupiga magoti na kuanza kuomba bali ni kutafuta ujuzi. Kwa maneno yangu hii sio kwamba ninawaangusha Manabii na Mitume ila nasema unapokuwa nje ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” linaoongozwa na mchungaji utakutana na manabii na mitume, lakini unapokuwa ndani ya kanisa la Mlima wa Moto unamsikiliza “One Person” ambaye ni Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwani Mungu amemua-“Anoint” akampaka mafuta na akampa neema ya kutangaza MAFANIKIO yako, na kwasababu hiyo ukiyashika anayosema utafanikiwa sana. Lakini leo nataka nifungue akili yako.


LAZIMA UJUE KUHESABU SIKU
Hutakiwa kuonekana umekakaa tu hueleweki, hujui utakufa lini? Utakwendaji? Na mipango yako ikoje?. Watumishi wengi sana hawapendi sana watu kuzungumzia kifo. Ni maombi yangu kipande hiki cha pili cha mwaka huu kikawe ni chema kwako, maisha yako yote yakapate kufanikiwa, na hizi siku zilizobaki hapa katikati Mungu akafanye mabadiliko, katika jambo ambalo ulibanwa hapa katikati uende ukapokee mpenyo wa kuchomoka hii.

Naomba usome Zaburi 90:12, 17. basi utujulishe kuzihesabu siku zetu tujipatie moyo wa hekima, na uzuri wa Bwana uwe juu yetu na nafsi ya mikono yetu ufanyie thabiti na kazi ya mikono yetu uithitishe. Ninaomba Mungu akupe moyo wa mafanikio. Unatakiwa kujiuliza wapi ume-“fail”

Kwanini Mungu anasema watu wamejeruhiwa mioyo, wamechoka? Hizo ni dalili kwamba Bwana amewabeba, na chochote unachokibeba kinauma, kinahuzunisha. Na hii inatokea hata kwa wachungaji kwani kila mwenye shida anatupia tatizo lake kwa mchungaji wake ili aweze kutatua kutokana na mamlaka na upendeleo aliopewa na Mungu, kwahiyo matatizo ya waumini wote wenye uhitaji anayabeba moyoni. 
Tusome Zaburi 6:4. “Bwana nijue jinsi nilivyo dhaifu” Je, umeshajiuliza utakufa lini wewe?, Ulishamuuliza siku za kukaa hapa duniani ni siku ngapi? Na ukishakufa, nani awalee hawa watoto wako? Mama ulishawahi kumuuliza Mungu kwamba, hawa watoto ulionao, utawafikisha sekondari au Chuo Kikuu na umri huu nilionao? Hapa mtunzi amesema, “Unieleze Mwisho wangu ni lini, siku zangu zimebaki ngapi?” Ezekia alipoambia hapa unaondoa mwanangu, Ezekia alikaa kimia akaangalia ukuta akaongezewa miaka 15.

Kumbuka ya kwamba jambo usilolifahamu ni sawa na usiku wa giza. Hutakiwa kutembeatembea kama mtoto mdogo anayekula pipi wakati una mzigo wa kusomesha wanao, kwasababu Biblia inasema, “Usiache elimu ikaenda bure” unatakiwa kusomesha watoto wako. Usifurahie tu kuzaa, unatakiwa kuangalia wataishia wapi? 
Unatakiwa kuhesabau siku zako za mbeleni na usianze kusema, “Eti mimi ninalazimishwa kuzaa?” Wewe mama siunajua kubadilisha kalenda ya kuzaa?, si ubadilishe sasa wakati baba anataka uzae. Nataka akili zako zifanye kazi.

Wewe ni mwana wa Mfalme, umebeba neema ya Mungu. Utakapoelewa siku zako za kuishi hautahofu chochote kitakachofuata. Kama utajua unasiki 50 za kuishi hapa duniani, hautaogopa malaria, wala kansa au chochote. Ayubu alipokuwa na mateso makubwa alisema, “My Redeemer lives” “Mtetezi wangu yu hai” kwasababu alikuwa anaelewa nguvu iliyopo.

Mtu yoyote ambaye anajua ana hekima na ana akili, mara nyingi anafanya vitiu vyake kwa utaratibu. Na wewe ukiwa na manung’uniko mengi na kusema Mungu hayupo ni kwasababu hujui utakufa lini. Lakini kwa wale wanaojua siku walizonazo mbeleni basi mikakati iliyopo wanajua hapa watapita kwenye zoezi na lazima wababrikiwe kwani Mtetezi wake yu hai, na huo ugonjwa unaomsumbau utayeyuka wenyewe, na mkopo wa SACOSS utayeyuka wenyewe.


Unatakiwa kujiamini na kusema, huwezi kufa kwa mkopo wa benki au kwa jambo lolote kwasababu Mtetezi wako yuko hai. Na ukitaka kufanikiwa katika mikakati yako lazima upate mkombozi wa fikra. Ndio maana unakuta mtu mwingine ambaye ni mwaminifu hawezi kutembea bila Mungu. 
Lakini kuna watu wengine wanajiishia hapa duniani na wanajiona wao kama makabeji hapa duniani, hawezi kufanya chochote na hawawezi hata kuheshimu uongozi. Sasa kwanini huwezi kumheshimu Yule mnyapala aliyewekwa na Mungu kwaajili yako. Na pengine unafikiria kama vile hakuna kifo. Ndio mana tunasema, umwambie Mungu akufundishe kuhesabu siku zako, halafu mwisho wangu utakuwa ni lini. Kama wewe ni “Part of Your Family, You Need To Think About That? Ukifika hatu ya kufikiria makubwa lazima utaishi wa “Discipline” 


Ninachoona sasa hivi kwa waumini wako Bishop Dr. Gertrude Rwakatare hawataki kusoma Biblia na wengine wanakuja kanisani kwa ku- “Beep”. Vitu vingine havieendagi kwa unabii bali unakwenda kwa kusoma, unakubali kufundishwa. Mungu mwenyewe anasema nendeni mkawafanya watu kuwa wanafunzi wangu Mimi, na kuwafundisha na kuwaamuru kuyashila yote.

Ndani ya mafundisho kuna uzima, utajiri, mali na akili. Sasa wewe kusoma Biblia husomi, mpaka umebanwa na malaria ndipo unakuwa karibu na Mungu.

Je, Utakufa Lini? Ukielewa siku zako za kufa, hautakula vyakula vyakula vya ovyo

SOMO LINAENDELEA...TUTAKULETEA