RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ROSE MUHANDO,ANGEL BENARD,CHRISTINA SHUSHO KUSINDIKIZA UZINDUZI WA DVD YA GOODLUCK GOZBERT



Mwanamziki wa Injili Goodluck Gozbert kutoka jijini Mwanza jumapili ya Tarehe 17.7.2016 atakuwa akizindua rasmi DVD yake mpya Iitwayo IPO SIKU.DVD hii itazinduliwa katika kanisa la TAG City Christina Centre(CCC) kuanzia saa saba kamili mchana.Sambamba na Goodluck Gozbert pia mwanadada Angel Benard na Christina Shusho na Rose Muhando watakuwepo katika concert hili.

Kiingilio Mlangoni ni Shilingi 20,000/= huku Clouds media Group kupitia kipindi chake cha Redio cha Gospel Trax ndio waandaaji wakuu wa tukio hili. Kuibuka kwa Goodluck Gozbert kwenye Muziki wa Injili kumeleta changamoto ya aina yake kwa kuwa aina ya muziki anaofanya imekubalika sana kwa vijana wa kikristo na hata wa dini nyingine. Lets go and witness kizazi kipya cha Muziki wa Injili.