Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya yalioandikwa ni huu utafiti kwenye gazeti la Nipashe chenye kichwa ‘Njia rahisi kufyeka vitambi ni hii’
Wakati maelfu ya watu duniani kote wakitambua kuwa njia maarufu ya kukabiliana na tatizo la kitambi na uzito mkubwa ni kuzingatia lishe bora na kushiriki mazoezi, imebainika kuwa njia nyingine ya kukabiliana na tatizo hilo ni kunywa maji kwa wingi.
Ripoti ya utafiti uliofanyika hivi karibuni juu ya uhusiano juu ya kiwango cha maji mwilini na uzito mkubwa, imefichua kuwa watu wazima wenye kawaida ya kunywa maji kwa wingi au kula vyakula venye majimaji mengi huwa na uwezekano mdogo wa kupata vitambi na kuwa na uzito mkubwa usiolingana na maumbile ya miili yao. Utafiti huo uliohusisha watu wazima takribani 10,000.
Kiongozi wa utafiti huo Dk Chang, ambaye ni profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha shule ya Afya Michigan nchini Marekani amesema…….>>>‘Wale wote ambao hutumia maji kwa kiasi kidogo walikutwa na uzito mkubwa zaidi kwa kipimo cha ulinganifu wa uzito wa mwili-BMI’s kulinganisha na wale ambao hunywa maji ya kutosha’
SOURCE: NIPASHE