RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE: MWANAMKE UJITUME, USIMDHARAU MUMEO ETI HANA PESA, IPO SIKU UTAABIKA AKIWA NA PESA

”Mwanamke lazima ujishushe kwa mwanaume.” Leo kapata anacheka lakini siku hana hela ananuna anaanza kulalamika na kusema, “Mtu hana hela, hana chochote, nyumba gani.” Kila nyumba ina siri tunasitiri, siri za nyumba zetu na wanaume wetu na wake zetu tunasitiri siri na hatulalamiki kwa sababu ya mikosi au kitu fululani, siku moja vitakwisha!!. Mama mmoja alikuwa na kazi nzuri, mume wake pia alikuwa na kazi nzuri, ikatokea yeye akapunguzwa kazi na mama akaendelea na kazi. Nyumbani yeye ndo akawa “house boy.” Siku moja mwanaume akashika gari la mke wake, akamwambia, “Usishike gari langu”. Usibadilike kwa sababu ya pesa, pesa ni makaratasi tu, usidharau kwa sababu ya pesa, hata uwe na pesa ngapi, ulizaliwa uchi utakwenda uchi hutobaki na chochote, hata ujenge majumba mangapi utaviacha duniani, hata uvae nguo kiasi gani utaziacha duniani, hata ulimbikize mapesa utayaacha duniani. Utakatifu na kuridhika kuna faida kubwa. Basi Yule baba akakaa miaka miwili (2) anatafuta kazi lakini hapati, kwa masimango mkewe anasema, “Hujapika, nimetoka kazini nimechoka hujapika?” Jamani hata uwe na pesa kiasi gani mume ni mume tu hata awe ni maskini yeye ni baba. Basi yule mama anamwambia hujafua nguo? Mume anajibu, “Mbona nimefua” Je, na zili zingine?” Anajibu, “Nitafua usiku” anamwambia, “Fua sahizi”. Jamani yamekuwa hayo? Kwakua wewe ni msomi!!??” Mwanaume ni mwanaume tu. Siku moja mwanamke akiwaa na mume wake alienda mahali, akakutana na wazungu, akawambia wazungu, “Namsindikiza mwenzangu”, mwanamke akamjibu mumewe, “Sioni sababu ya wewe kukaa hapa, unanielemea tu, umekuwa mzigo kwangu.” Mwanaume wa watu akaenda, akazungukazungu akarudi na wale wazungu wakampenda wakamuajiri wakamnunulia shangingi, akapewa mshahara, akapewa dolla elfu10 kwa mwezi. Baada ya kupata zile pesa akaenda nazo kwa mke wake nyumbani, akazimwaga zile hela mezani, akasema, “Njoo chumbani umeziona pesa, hizi pesa ndio mshahara wangu wa mwezi mil.20.” Mwanamke akasema, “Nenda zako umeziiba”, mwanaume akasema, “kama kuiba rahisi na wewe si ukaibe?” Yule mwanamke akaenda kukaa kwanza sebuleni, akaanza kujipendekeza kwa mume akisema, “darling, baby, nikuletee kinywaji basi!!??”. 

“Aliye juu mgoje chini” uliyemsimanga siku moja Mungu atamuinua ndio maana nikasema “waume kaeni na wake zenu kwa akili.” Leo hii yule mwanaume aliyedhauriwa na mke wake kwa kukosa kazi na kuanza kumpikia mke wake na kufua nguo zake kwa kusemwa vibaya ndani ya nyumba, anapokea  mshahara wa mil.20 na amepewa shangingi ya kutembelea, wakati mke wake anapokea mshahara wa mil.2 kwa mwezi. Ridhika na ulicho nacho, turidhike na hali tulizo nazo. Uwe nacho usiwe nacho mshukuru Mungu lakini usiibe kwa sababu unataka vitu vya hali ya juu. Msichana anataka simu kubwa kama ya mwingine, anataka na yeye awe na laptop, IPad, anataki vitu kwa wepesi na hujui kuwa kuna chatu mbele yako baada ya kuvipata hivyo kwa njia isiyo halali, atakumeza tu na utaabika kwa wenzako. Vyote vitakuja kwa wakati wake. Kasichana kadogo kanisani kanaimba kwaya utakuta kanamimba, ukikauliza, kanasema “unajua shetani alinipitia,” wewe huyo sio shetani bali ni tamaa zako na wamekupachika mimba na wamekuacha, umetemwa kama bigijii iliyoisha utamu mdomoni au umetupwa kama vocha iliyotumika, haifai tena hata kuangaliwa, inakanyagwa tu na wapita njia? Shetani gani amekuambia ukale chipsi za mwanaume? Eti na mimi nilikuwa na njaa nikaenda nae mwanaume kula chips na baadae nikaenda naye kwake. Nasema “hiyo roho ishindwe kwa jina la Yesu.” Katika matatizo katika shida simama na Bwana utakatifu na kuridhika ndio utamuona Mungu. Mwambie mwenzako, “ridhika na ulicho nacho mungu ataleta vizuri kwa wakati wake.”

Ukiona mtu anaendesha gari mpya usichanganyikiwe maana kesho yako inakuja utaendesha. Usione mtu kajenga nyumba nzuri ukaanza kunung’unika bali mwambie Mungu “najua unaniwazia mema”.

Hivi ndivyo Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alifundisha Jumapili 19.08.2016