RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE: NI BORA KUWA NA MALI CHACHE UKIMCHA MUNGU BILA MANUNG’UNIKO

Soma Mithali 15:16, “Kuwa na mali chache pamoja na kumcha Bwana ni bora kuliko kuwa na mali nyingi pamoja na taabu”. Hatukatazi watu wawe matajiri , mimi kama Bishop wako Dr. Gertrude Rwakatare naambukiza watu wawe mabilionea. Nasema, “Jaribu kwa hali na mali katika biashara yako unifikie hata nusu, kama si nusu basi hata robo”. Nataka kila mtu awe na furaha kwa maana pesa ndio sabuni ya Roho. Ukitaka kitu kizuri lazima utoe pesa huwezi kunena kwa lugha dukani, ni lazima uwe na fedha ndo upate nyama. Kwahiyo kwa hali uliyo nayo, muombe Mungu ili aweze kukufikisha mahali wenzako wamefika katika maendelea. Upo kwenye foleni, zamu yako itafika na utafurahi. Watu wamejaa kunung’unika eti maisha magumu, sawa maisha magumu lakini sisi si sawa na wamataifa, lazima tujipe moyo kwamba Mungu wetu anaweza nasi siku moja atatuongoza. Naona pesa mbele yangu, naona mafanikio fedha na dhahabu. Mali tunazoziona ni mali za Baba yetu usianze kunung’unika kwasababu Mungu yupo kazini. Mungu hawezi kukuacha anasema, “Njoeni kwangu nam nitawapumnzisha”. Mwamini Mungu, tumejifunza IMANI, simama na Neno. Lakini usiweke manung’uniko. wana wa Israel walikufa wengi jangwani, wana wa Israel wengi hawakuingia jangwani kwa sababu ya manung’uniko. Umekuwa na malalamiko kwa sababu ya kujilinganisha na watu. Huna haja ya kujilinganisha na nyumba fulani, usimulinganishe mume wangu na mtu mwingine. Unaanza kusema, “Baba fulani mimi naona anajitahidi sana, kishanunua gari, unaona anavyovaa, ana simu ya kupangusa wakati mimi bado nina kitochi. Ridhika na simu ya tochi ili mradi unapata mawasiliano. Katika maisha kuna kupanda na kushuka. Huu ni ujumbe aliohubiri Jumapili 18.09.2016 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Kanisania Mlima wa Moto Mikocheni ”B