RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAMA AMSHUKURU MUNGU NA WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO KATIKA KIPINDI CHA KUMUUGUZA DADA YAKE MPAKA UMAUTI WAKE

MAMA AMSHUKURU MUNGU NA WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO KATIKA KIPINDI CHA KUMUUGUZA DADA YAKE MPAKA UMAUTI WAKESiku ya Jumapili 18.09.2016 mtumishi wa Mungu alikuwa na haya ya kusema, “Neno la Mungu linasema shukruni kwa kila jambo. Jambo nililo kutana nalo, na leo nimekuwa mzima ni muujiza tu. Kweli niliondokewa na dada yangu mpendwa nilimpenda sana. Nimesimama mbele za kanisa na mbele za Mungu ninasema, “asante kwa sababu kanisa lilisimama pamoja na mimi kujari famili ya yangu.” Napenda kumshukuru Mungu sina kitu nachoweza kusema sana nawaombea kwa Mwenyezi Mungu yeye ndiye anayeweza kutufikisha hapa kwenye hili kanisa la Mlima wa Moto MIkocheni “B”. Asante kwa sababu ya hili kanisa nimepata nguvu. mama Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alisimama na mimi tangu mwanzo nasema, “asante Mungu kwa kunifikisha kwenye nyumba hii nimepata wazazi, kwenye kipindi chote kigumu walikuwa pamoja na mimi.” Mungu awabariki sana.” 

Na badae ndugu wa marehemu ( katika picha ya kwanza , wa pili kutoka kushoto) alikuwa na haya ya kusema “Ninazo shukrani za pekee kwa mama Askofu Gertrude Rwakatare ninasema Mungu ambariki mno “Mama wa Faraja,” ni “Mama wa Upendo” ni “Mama asiyekuwa na mfano.” Faraja yake imekuwa ni yakipekee, Mungu alibariki kanisa la Mlima wa Moto, awabariki wote azidi kuliongeza kanisa na kulibariki, tunamshukuru wote kuanzia Mch. Noah Lukumay na mke wake, wazee wote wa kanisa, viongozi wote washirika wote pande zote tunasema Mungu awabariki kweli mahali hapa ni mahali pa faraja. Mungu awabariki.” Hii ni baada ya kufiwa na ndugu yake mpendwa.