Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema serikali yake inajiandaa kujenga uwanja mpya wa kisasa wa ndege utakaogharimu dola za Kimarekani zaidi ya milioni 800. Uwanja huo utakuwa mkubwa na wa kisasa kuliko uwanja wa sasa wa Kigali International Airport uliopo jijini Kigali.
Hatua hiyo ya serikali ya Rwanda ni maalum kwa ajili ya kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kuhudumia ndege nyingi kwa wakati mmoja tofauti na sasa ambapo uwanja huo hauna uwezo wa kuhudumia ndege nyingi kwa wakati mmoja.
Serikali hiyo inataka kwenda sambamba na nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki ambazo zinapanua au kujenga viwanja vipya ikiwemo nchi ya Tanzania.