23.2016.2016: MARTHA MWAIPAJA ATOA UJUMBE MZITO SIKU YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"
Martha Mwaipaja
Siku ya Jumapili 23.10.2016 mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Tanzania martha Mwaipaja alikuwa na haya ya kusema na waumini wa Mlima wa Moto Mikocheni “B” alisema, “Wangapi wataiona kesho? Usikatishwe tamaa na dunia hii. kuna Mungu anayekujua kuliko yeyote yule. Mungu haangalii mavazi wala kujipamba kwako.
Martha Mwaipaja akipokea zawadi kutoka kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wakati akiimba
mnajipamba sana lakini yupo ambaye ameshikilia maisha yetu. Unajua kuna mwingine anaweza akaona kama hana thamani kwa sababu ya hali anayoipitia, lakini sikiliza, hivyo ulivyo utaona mkono wa Mungu kwako. Yesu Kristo alikubali kupigwa ili akupate wewe. Yupo Mungu anayejua kesho yako usikate tamaa usilie, kuna mahali unaelekea”.
Baada ya kumalizakuongea hayo Martha Mwaipaja aliweza kuimba na baadae Mzee wa Kanisa Mch. Mama Mgetha alikuwa na haya ya kusema, “Tumemuona Bwana kupitia wimbo wake. Kila aliye katikati yetu hapa kama wewe ni Mkurugenzi, kuna mahali umetoka, Martha Mwaipaja wakati anaimba wimbo huu nikamshangaa Mungu akinihudumia.
Nikwambie mpendwa Mungu anasema, ”Alivyojuu sana njia zake zipo juu”. Nakumbuka nikiwa binti mdogo nilikuwa nalima kibarua mahali fulani, kuna mzee mmoja kijijini alinipa kibarua cha kulima akanihesabilia hatua 30 kwa Tsh.30.
Nilipomaliza kulima nikapewa pesa, nikanunua daftari, pen kwaajili ya shule. Leo nikiingia kijijini nipo na gari V8, jamani kumbe ni Bwana. Mwanadamu asikukatishe tamaa maisha yako mikononi mwa Jehova hata wewe hujafika mwisho. Yupo Mungu yeye ni Mwanzo na mwisho, yeye ni Alfa na Omega. Martha Mwaipaja Mungu akubariki sana”.
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akicheza na mzee wa kanisa Mama Mshobozi