NECTA: Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba uliofanyika Septemba 8 na 9, 2016 huku jumla ya watahiniwa 795,739 walisajiliwa kufanya mtihani huo.
Akizungumza mbele ya wanahabari, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Charles Msonde ameeleza kuwa ufaulu wa wanafunzi umeongezeka kwa asilimia 2.52 ukilinganishwa na ule wa mwaka jana (2015).
Shule iliyoongoza kitaifa ni shule ya Msingi Kwema iliyoko mkoani Shinyanga.
Kuyatazama matokeo ya darasa la saba mwaka 2016;