RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAAFALI YA WATOTO WA SHULE YA AWALI ST. MARY’S JUNIOR INT. SCHOOL YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM.

Siku ya Jumamosi 26.11.2016 wanafunzi wa Shule ya Nursery ya St. Mary’s Junior Int. School iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam, waliweza kufanya maafali ya kumaliza masomo yao ya awali. Mkurugenzi wa shule za St. Mary’s Int. Schools Tanzania Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa na haya ya kusema, “Niwashukuru na kuwapongeza watoto hawa kwa kumaliza elimu yao ya awali siku ya leo, niwashukuru wazazi wa watoto hawa kwa kuwasomesha, niwashukuru walimu na wafanya kazi wa Shule ya St. Mary’s Junior Int. School kwa kuwafundisha na kuwalea watoto hawa, nimshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kuwalinda watoto hawa na kuwapa uzima mpaka siku hii ya leo. 

Wazazi ninachotaka kusema juu ya shule yetu ni kwama, sisi tunauzoefu wa kufundisha kwa muda wa miaka 20, wazungu wanasema “Old is Gold”. St. Mary’s Int. Schools ni waanzilishi wa “English Medium Schools” tangia mwaka 1996 mpaka 2016. Tunasema pia “Quality is Our Motto” , hatuaacha kuzingatia kutoa “quality” ya “product” tunayotoa. Nataka nisema ya kwamba, “Hakika ukimuleta mto St. Mary’s Int. School” umemleta mahali sahihi. Nakuomba kama mzazi usibabaishwe na majina ya shule zingine wala usisikilize maneno mengi kutoka kwa watu. Watu wengine baada ya kufanya kazi nzuri katika shule zao, wao wamebaki kuchafua shule za wenzao, lakini sisi kama St. Mary’s Int. School tunasema, “St. Mary’s Int. School number one”.
Katika matokeo ya darasa la saba, St. Mary’s Int. Schools zote Tanzania nzima imeshika nafasi ya “10 Bora” katika wilaya kwa kufaulisha wanafunzi. Mkoani Mbeya imekuwa ya namba moja (1) Kiwilaya na imekuwa ya tano (5) Kimkoa. Shule ya St. Mary’s Mbagala Int. School na St. Mary’s Kihonda Morogoro zimekuwa namba mbili (2) ki Wilaya, Shule ya St. Mary’s Ifakara Int. School iliyopo wilaya ya Kilombero Kiwilaya imekuwa ni ya tatu (3), lakini kwa miaka miwili mfululizo shule ya Ifakara imekuwa ya kwanza Kimkoa nay a kwanza Kiwilaya, shule ya St. Mary’s Tabata Int. Schools na St. Mary’s Mwanza Int. Schools imekuwa namba sita (6) Kiwilaya. Katika shule za kata St. Mary’s Int. Schools imekuwa ikishika namba sita (6), shule ya St. Mary’s East Africa Mikocheni imekuwa namba nane (8) katika wilaya ya Kinondoni na shule ya St. Mary’s Junior Int. Schools ambayo leo inafanya “Graduation” imekuwa namba kumi (10) Kiwilaya. 
Ningependa kuwapongeza walimu wa shule zote za St. Mary’s Int. School, Mungu awabariki, awazidishie kwa upendo wenu wa kuweza kutufundishia watoto wetu kwa moyo. Ninapenda kusema ya kwamba, “Kufauku kwa st. Mary Int. school” ni wa uhakika”. Kuna shule zina majina makubwa lakini hawafaulishi, lakini shule yetu wote wanafaulu na wanachaguliwa.
Huduma zetu kila mtu anajua kuwa ni nzuri. Kuhusu usafiri: Kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakilalamika kuwa shule wanazosomesha watoto wao wamekuwa wakilaamika mfumo mzima wa usafiri wao kuwa ni mmbaya, lakini sisi Mungu ametusaidia mfumo wa usafiri ni bora.
Nataka kukuhakikisha kuwa tumeamua kusomesha wanafunzi wa Kitanzania, kwani majengo yetu ni ya uhakika, elimu ni bora, walimu wetu ni wa uhakika, kufaulisha inaongoza. Shule zetu ni za siku nyingine lakini zipo TOP yaani ziko katika nafasi za juu katika ufaulishaji.
Kuhusu ada yetu kwa wanafunzi ni ya kulipika, kwani ada yetu kwa wanafunzi ni Tshs. 1,700,000 na unaweza kulipa kwa awamu nne au mbili. Huwezi kupata shule yeyote yenye ada ya chini kama St. Mary’s Int. Schools. Kwanini ulipe pesa nyingi kwaajili ya ada wakatika shule yako inayofaulisha ipo na kwa gharama nafuu kabisa. Kulipia Boarding ni Tshs. 2,100,000 na unaweza kulipa tshs. 500,000 kwa vipindi vinne mpaka unamaliza deni lako. Je, utapata wapi shule inayoweza kuvumilia kulipa ada kwa laki tano tano.
Sisi kama St. Mary’s Int. Schools tumekuwa tukielewa kuwa upatikanaji wa fedha ni mgumu kwahiyo kama shule ikafanya jitihada ya kumtafuta mfadhili ambaye atatulipia usafiri na chakula, kwahiyo sasa tumebakiza issue ya ada kwako wewe mzazi kulipia. Na mimi mmiliki wa shule za St. Mary’s Bishop Dr. Gertrude Rwakatare nitaendele kutafuta wadhamini wengine ili watusaidie katika suala zima la ada, na Mungu akitusaidia kuwapata basi unaweza kulipia ada yako chini yah ii unayolipia kwa sasa. Mwanafunzi wako akikaa Boardingi ni rahisi zaidi kulikoa angetokea nyumbani kwako na kuja shuleni kila siku. 
Unajua tofauti ya ada ya mtoto alyeyoko Boarding na aliyoko Day ni Tshs. 100,000 tu. Unapomuweka mtoto Boarding anaweza kuwapata walimu wake asubuhi, mchana, Jioni na usiku pale tu anapowahitaji. Mtoto najengaa katika ile “Academic Spirit”, anakuwa na ule moyo wa kupenda kujisomea vitabu kila wakati. Kwahiyo naomba sana mlete mwanao Boarding kwani kuna vitanda vizuri, mashuka mazuri, matron wazuri (watoto wako watatunzwa vizuri). Watoto wetu wa boarding milo yao ni mitano (5). Kwa mfano wa wanafunzi wa Nursery waliopo boarding asubuhi anakunywa uji, saa nne (4) wanakunywa uji na mkate. 
Na mwisho kabisa ningependa tena nikualike uwalete watoto St. Mary’s Int. Schools. Kama unawatoto wanasoma kwingine naomba sasa uwalete hapa shuleni ili wasome eneo moja. Tumeanza kuandikisha watoto watakaoanza January 2016, tunawakaribisha sana na Mungu awabariki.

Kama mchungaji ninaomba niombe kwaajili ya wazazi wetu, kwani kuna magonjwa, kuna kufukuzwa kazi, kunakutumbuliwa na kuna mambo kadha wa kadha, sasa tuombe Mungu awaepushe, na wazazi wa St. Mary’s Int. Schools wasiangamie katika hayo. Kwa kumheshimu Mungu basi weka mikono yako miwili kifuani, na inamisha kichwa chako. Tuombe, “Baba yetu wa mbinguni, ninaweka watu hawa mikononi mwako, uwalinde na ajali mbaya, magonjwa mabaya, uwawezeshe kupata pesa kwaajili ya kuwasomesha watoto wao, kwa wale waliotengana ninaomba ukatengue utengano wao ili wawe wamoja waweze kuwalea watoto wao na kuwasomesha. Ninakemea na vifo vya desemba vitoke kwa jina la Yesu . 
Tunajifunika kwa damu ya Yesu, ulinzi uwe mbele na nyuma. Ninawaweka na hawa watoto waliomaliza masomo yao ya Nursery siku ya leo mikononi mwako Baba. Wamehitimu shule ya awali na sasa wanaingia shule ya msingi, ninaomba Mungu uwalinde na magonjwa ya kitoto, walinde na michezo mibaya. Baba Mungu ninaomba wakue wawe watoto wazuri. Kama watoto wenyewe walivyosema kuwa wanataka kuwa madokta, marubani, Marais na vyeo mbalimbali. Wabariki watoto hawa, wageni, wazazi, wafanyakazi, na walimu kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu..Amen