25.12.2016: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ATOA UJUMBE MZITO SIKU YA KRISMASI ATAKA UTAMBUE UTAFANYAJE KUENDELEA NA MAISHA YA KUMTUKUZA MUNGU BAADA YA KUZALIWA KWA YESU KRISTO
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Krismasi 25.12.2016
aliweza kutoa ujumbe mzito sana wa kuzaliwa kwake Yesu Kristo, alikuwa na haya
ya kusema, “Unajua mamajusi walitoka mbali kuja kumuona mtoto Yesu. Yesu
alikuja ili aweze kukaa na wanadamu. Sasa leo Yesu amezaliwa ili akae na
wewe.
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
Yesu amezaliwa sasa inatakiwa
uendeleeje na huyu Yesu? Unatakiwa kumshika huyu Yesu katika maisha yako. Yesu
amezaliwa na ameingia moyoni mwako, na sasa anakaa na wewe. Yesu ni mgeni rasmi
katika nyumba yako siku ya leo ya Krismasi. Soma kitabu cha Luka 2:41. Sisi
tunajiita Wakristo kwasababu tumempokea kuwa Bwana na Mwokozi wetu. Siku ya leo
Kristo anataka kukaa pamoja na wewe.
Furaha Isaya na Rose Rwakatare (kulia)
Ukimpokea Kristo anasema Yeye Baba anakaa
ndani yetu. Lakini watu tunavyosherekea Krismasi tunakuwa ni watu tunayepokea
mambo juujuu na sio mambo ya ndani. Sasa kwasababu Krismasi hii ni mwaka mpya
Kiroho,basi andika “My New Year of Resolution” andika malengo yako na matakwa
yako, andika yale ya mwaka jana yaani 2016 kuwa ulishindwa nini? Mahudhurio
yako ya ibada yalikuaje?. Kipindi cha Krismasi ni cha kufanya “Spiritual
Inventory”
Miriam Jackson akisoma neno
Mch. Elizabeth Lucas
Mwenye duka mara nyingi hukaa kwa wiki mara moja kuangalia
ni mali gani inaisha kwa haraka katika duka lake, na katika kwenda kununua vitu
vya dukani anaangalia kile kinachouzika sana. Na wewe wakati wa Krismasi ni
wakati wa kutengeza upya kiroho chako, ni wakati wa kukarabati maisha yako ya
kiroho, ni wakati wa kumwambia Mungu ninaomba unipe nguvu mpya ya kuanza
kiroho.
Wazazi wa Yesu walikuwa wamemzoea Yesu, kwasababu ni mtoto
wako, wakaingia naye kama ilivyo desturi katika eneo la kuabudia na wakaabudu,
walipomaliza kuabudu, wakaanza kurudi walikotoka wakijua Yesu ypo katikati ya
jamii.
Wazazi wake wakaenda mwendo wa siku tatu wakiwa wamemsahau mtoto wao
(Yesu). Sasa sijui na wewe una miezi mingapi umemsahau Yesu, eti kwasababu
umekwazwa. Watu wengi sana wamekwazwa na wakiambiwa twende kanisani wanasema,
“Achana nayo, maombi ya nini bwana?” Sasa na wewe unatakiwa kujiuliza umemuacha
Yesu kwa ahatua ngapi?
Watu wengine wanaamua kuzila kuja kanisani kusali, kumuomba
Mungu, kukutana na watakatifu wenzao wanabaki majumbani mwao na wengine
wanasema wao wanasali kwenye TV. Na hii ni kutokana na kukwazika na
kumesababisha kuumia moyoni mwake.”
Watu wengine wanampokea Yesu na wanaishi naye kwenye maombi,
kwenye kusifu n.k lakini watu hao hao wana “private live”, na wengine
wanadiriki kusema, “Nina maisha yangu ya siri”, nina vitu vinenge sitaki Yesu
aviguse.
Mtu huyo ambaye anasema yeye ana “Private Live” akikabwa anaanza
kumtafuta Yesu. Watu wametenga maeneo Fulani ya kuficha viasira vyao, nap
engine ni kiasira cha Kikulya au cha Kinyakyusa. Utakuta mtu huyo amepiga
magoti kusali lakini ndani yake amesimama, na pengine anakung’ong’a.
Ni lazima tuvue utu wa kale na tuvae utu upya. Wakati wa
Krismasi ni wa kukaa karibu na Yesu. Na watu wengine wakishabanwa mahali na
mambo ya dunia wanaanza kusema Yesu “Im Sorry”. Kama tumeamua kuokoka na
kumpenda Mungu basi tumpende Mungu kijumla na mia kwa mia, kusiwe na mahali pa
kubakiza katika kupenda Mungu.
Watu wengine wakimuona Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
amependeza wanaanza kuniuliza, “Eti wewe unapendezaga kwaajili ya nani?” na
mimi nawajibu, “kwaajili ya Yesu”, wananiuliza tena, “Yesu unamuona?”,
nawajibu, “ndio namuona”.
Krismasi hii muache Yesu maisha yako, mwambie Yesu ingia
ndani ya moyo wangu, ingia kazini kwangu, ingia kwenye nyumba yangu, ingia
kwenye ndoa yangu, ingia kwa watoto wangu, Mungu ingia kila mahali na sina
mahali ninapoficha mabaya yangu. Ukifanya haya yote na zaidi hapo ndipo Mungu
anakuwa pamoja na wewe. Mungu amekuja ili akae na wanadamu na kuwasaidia.
Hakuna mtu aliyekaa katika Ukristo na akajuta, lakini
anayejuta anakasoro katika Ukristo wake. Nataka nikwambie kuwa kwa Yesu kuna
raha, kuna pumziko la kweli, kuna amani ya kweli. Wenzako wanakunywa pombe ili
wapate amani lakini wewe unapata amani bure kabisa.
Amni ya Yeu ni “Permanent”,
amani ya Yesu haina majuto lakini amani ya pombe lazima utapigana na mtu,
utamaliza pesa na asubuhi unaanza kuhangaika chakula cha kulisha watoto. Amani
ya kutafuta ndani ya chupa sio amani ya kweli, ni amani yenye majuto. Nakuomba
uje kwa Yesu kwani yeye atakupa amani ya kudumu na ya kweli, utakuwa na furaha
hata kama unauzuni.
Yesu anasema usinione haya mbele za watu, na mimi nitakuone
haya mbele za Baba yangu. Watu wanaona haya kusema, “Mimi Nimeokoka”. Mwingine
anaposimamishwa mbele ya watu wakubwa na wenye fedha zao, anaogopa kusema,
“Mimi ninasali kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare”.
Ni lazima utangaze msimamo wako wa kiimani ili watu wajue.
Unatakiwa kuinua bendera ya Yesu ili watu wote wajue kuna walokole katika ile
nyumba. Mungu akubariki sana.
Miriam Jackson akisoma neno
Mch. Elizabeth Lucas