RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

23.01.2017: EMMANUEL PETER (SMARTBOY) AMASHUKURU BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE KWA KUPATA KIBALI CHA KUWAHUDUMIA WATU KWA NJIA YA UIMBAJI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


Katika watu waliopewa neema ya uimbaji duniani huwezi kumsahahu kumtaja Emmanuel Peter (Smart Boy). Kuna kitu Mungu ameweka ndani yake ambacho kinaokoa maisha ya watu kuoka katika mateso makubwa ya shetani. Emmanuel Peter (Smart Boy) ni moja ya watu waliokuwa watukutu na wakishanda kwenye vigodoro na kuvuta bangi, lakini siku moja alisikia jina hili lishindalo majina yote la Yesu Kristo ndipo alipoamua kuokoka na sasa anamtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.

Siku ya Jumatatu 23.01.2017 ikiwa ni siku ya pili ya semina ya siku 8 za KUVIKWA NGUVU NA BWANA katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Emmanuel Peter alimshukuru sana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kupata kibali cha kusimama katika madhabahu ya Mungu ya Mlima wa MOto Mikocheni "B" na kuweza kuimba. Wakati anaimba nyimbo inayopendwa na walio wengi ya MUNGU NI MUNGU TU watu walionekana kuguswa na ujumbe aliokuwa akiutoa pamoja na zile hisia za uimbaji wake. Baadhi ya maneno yaliyomo katika wimbo wake yanasema hivi, 

“Hapa duniani nimezunguka, na katika safari zangu zote sijaona mwenye upendo kama huu wa Mungu. Anayejua kupenda ni Mungu na akikupenda kweli hakuna atakaye kukuumiza. Upendo wa Mungu si kama wa mwanadamu kwani mwanadamu akikupenda leo kesho anakuchukia lakini Mungu wetu wa mbinguni yeye ndiye mwenye upendo wa kweli. Mungu anajua kupenda, anajua kujali kuliko mtu anavyomjali mke/mume wake. Upendo wa Mungu ni wa tofauti, upendo wa Mungu wangu ni wa gharama, upendo wa Mungu si wa mume na mke bali upendo wa Mungu, upendo wa Mungu si kama wa mama kwa mtoto bali upendo wa Mungu ni wa tofauti.

Huyu Mungu aliupenda ulimwengu baada ya kuona mwanadamu amekosea akamuagiza mtoto wake Yesu kutuokoa. Kila mmoja kupitia Yeye akasamehewa dhambi zake. Kuna watu wengine wanaua watoto wao kwa faida zao wenyewe na sio kwaajili ya watu wengine, ila ni Mungu tu anayejua kupenda.” Huo ndio ujumbe wa mwimbaji Smart Boy ambao unapatikana katika albam yake ya NI MUNGU TU. Kumbuka semina hii itahitimishwa siku ya Jumapili 29.01.2017