RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MMILIKI WA FACEBOOK AMSIKITIKIA TRUMP KUWAZUIA WAHAMIAJI KUINGIA MAREKANI



Mark Zuckerberg na Mkewe.

MMILIKI wa mtandao maarufu wa kijamii duniani, Facebook, Mark Zuckerberg amesikitishwa na kauli ya rais mpya wa Marekani, Donald Trump ya kuwataka wahamiaji hasa wale wanaotoka nchi za Kiislam za Afrika ya Kati na Mashariki wasiingie nchini Marekani na hata waliomo wafungashe vilago vyao na kurudi makwao.

Kupitia akaunti yake ya FACEBOOK, Mark ameeleza kusikitishwa kwake na kauli hiyo ilihali chimbuko lake siyo Marekani na hata mkewe, Priscilla wazazi wake walikuwa wakimbizi kutoka China na Vietnam.