RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JINSI YA KUTIBU FANGASI UKENI


WANAWAKE wengi wana tatizo la fangasi kwenye uke, lakini hawajui namna ya kulitatua kwa njia za asili. Tiba ni nyingi ambazo unaweza kufanya ukiwa nyumbani kwako. Wengi huwashwa na wengine hupatwa na kupata uvimbe sababu ya kujikuna wanapopatwa na ugonjwa huu unaosababishwa na bakteria wanaoitwa Fungus Candida.

CHANZO CHA TATIZO
Antibiotics, hutumiaji wa mara kwa mara wa dawa hizi husababisha mwanamke kupata tatizo hili. Vitu vingine vinavyosababisha ugonjwa huu ni ujauzito, ugonjwa wa kisukari, ulaji mbaya na baadhi wakikaribia kuingia kwenye siku zao, mawazo na kutopata usingizi.

TIBA ASILI
Wengi hutumia maziwa ya mgando kama tiba, kwani yana bakteria wanaosaidia kuweka sawa ukeni. Baadhi hunywa kawaida na wengine huyagandisha na kuyaingiza ukeni. Kitunguu swaumu nacho ni Antifungas.Kitunguu kimoja kikubwa fresh, kimenywe kisha kifunge kwenye kitambaa kilaini sana na kukiingiza ukeni wakati wa kulala.

Asubuhi kitolewe. Limao au siki hutibu kwa mgonjwa kunyunyizia maji yake yaliyochanganywa na maji ya kawaida kwa kuosha sehemu ya uke yakiwa vuguvugu. Wagonjwa wanashauriwa kutofanya mapenzi kwani wanaweza kuwaambukiza wenza wao, wapendelee kunywa maji mengi wakati wa kulala na kuvaa nguo za kotoni.