Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga, akizungumza na wanahabari. Pembeni yake ni viongozi wa tume hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendela.
Wanahabari wakichukua matukio.
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora leo imelaani ufukuaji makaburi ya watu wenye ualbino.
Hayo yamesemwa na wadau mbalimbali kwenye mkutano uliojadili ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ualbino uliofanyika katika ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam.
Mambo mengine yaliyojadiliwa ni unyanyasaji wa watu wenye ualbino na namna ya kukemea tabia hiyo miongoni mwa watu wachache wenye tabia hiyo ya kinyama.
Akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa mkutano huo, mwenyekiti wa tume hiyo, Bahame Nyanduga, alisema kikao hicho kililenga hasa kukemea matukio yote ya kufukua makaburi na kuwaomba wananchi kutoa taarifa wanapoona viashiria vya watu wenye muonekano wa kufanya mambo mabaya.
“Tunatoa rai kwa wananchi na wadau kushikamana ili kutokomeza vitendo vya kufukua makaburi ya watu wenye ualbino kama tulivyoshikamana kipindi cha nyuma kulipokuwa kumekithiri matukio ya kuwaua watu ualbino,”alisema Nyanduga.