25.06.2017: WATU WAPOKEA NGUVU ZA MUNGU KUPITIA MAOMBI YA KUONDOA NJAA YALIYOFANYIKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI
//Jijengee tabia ya kufanya maombi kila kuitwapo leo//
//Tamani kuongozwa na Roho Mtakatifu kwa kila jambo unalofanya//
//Maisha yako yawe ni maisha ya IMANI//
//Kila unaloomba amini Mungu ameshalipokea na kulijibu//
//Ondoa mashaka kwa kile unachoomba//
//Maombi yana nguvu kwa mtu anayemwamini Mungu//
//Omba ukimaanisha na sio kufuata mkumbo//
//Muombe Roho Mtakatifu akufundishe kuomba//
//Omba katika Roho wa BWANA//
//Waamini watumishi wa Mungu kwa kila jambo wanalokuambia, UTAFANIKIWA//
//Usikubali muda wako ukapotea bila ya kuomba//
//Jitahidi kuwa na maisha ya kumuamini Mungu//
//Mwabudu Mungu katika Roho wa kweli//
//Baada ya kumaliza maombi yako, sema "Asante Yesu" kwani yeye ndiye aliyekupa kibali cha wewe kufanya maombi hayo//
//Kila jambo unalofanya anza kwa maombi na maliza kwa maombi//
//Omba Roho Mtakatifu akuongoze kwa kila jambo unalofanya na hatua unazopitia latika maisha yako//
**********************************
Siku ya Jumapili 25.06.2017 katika ibada ya maombi ya KUONDOA NJAA majumbani mwetu iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", watu wa Mungu walipata nafasi ya kufanya maombi kwaajili ya maisha yao. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiongozwa na Roho Mtakatifu aliwaomba watu kushikana na kufanya maombi kwaajili ya maisha yao. Kila mmoja aliweza kumuombea mwenzake na kumkabidhi mikononi mwa Mungu ili atawale maisha yake. Maombi yalikuwa ya baraka sana kwa kila aliyefika katika ibada hii.
Ibada hii ilikuwa ni ibada uliyotawala uwepo wa Mungu. Watu walifunikwa na wingu la Mungu na pia uwepo wa Mungu ulitanda kanisa zima. Watu walipokea nguvu mpya kutoka kwa Mungu hasa wale walioamini kile wanachokiomba mbele ya Mungu wetu wa mbinguni.
Najua ulitamani kushiriki ibada hii lakini kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wako ukashindwa kufika ibadani. Pengine ulikuwa unaumwa, uko jela, umekatazwa na mkubwa wako wa kazi, unauguza, ulikuwa safarini, ulipata ajali ukiwa njiani kuja kanisani na sababu zingine kama hizo, nataka kukuambia kuwa nafasi bado unayo, jitahidi Jumapili na katikati ya wiki kufika kanisani Mlima wa MOto Mikocheni "B" kwani kuna baraka zako ambazo Mungu amekuandalia kupitia watumishi wake.
Mungu bado anakupenda na ndio maana anazidi kukulinda hapo ulipo. Kwahiyo na wewe jitahidi kuonyesha mapenzi yako kwake kwa kufika kanisani na kushiriki ibada zilizojaa UPAKO wa aina yake. Acha kusikiliza sauti inayosema "USIENDE KANISANI" hiyo sauti ni ya shetani na ikimbia kabisa.
Mungu anakuita "NJOO", anakuhitaji kwa kazi yake, anakuhitaji ili abadilishi maisha yako, anakuhitaji ili umtumikie, anakuhitaji ili ukafanyike baraka kwa watu wengi, anakuhitaji ili siku yako ya kuondoka hapa duniani mkaonane mbinguni.
**********************************
//Bishop Dr. Gertrude Rwakatare//
//Mlima wa Moto Mikocheni "B"-Dar es Salaam Tanzania//
//Ibada Jumapili ni saa 3 asubuhi - saa 8 mchana//
//Usafir ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho -DSM au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola utaona magari yetu//