25.06.2017: TUKUPONGEZE ULIYEFIKA KATIKA IBADA YA JUMAPILI YA KUONDOA NJAA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"
Inapendeza kuona watu wanamkumbuka Mungu wao aliowaumba kwa kufika kanisani na kushiriki ibada Takatifu. Mungu anafurahi sana kuona watu aliowaumba wanamtumikia kwa bidii na kwa kujituma, hawakosi kuhudhuria ibada za kila Jumapili katika kanisa lake takatifu. Mungu anaguswa na jitihada zako za kumtafuta na kumtukia. Umefanyika baraka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Wewe ni nguzo ya kanisa hili, na Mungu atakubariki mpaka maadui zako watakapokushangaa
Tunazidi kukushukuru wewe ambaye siku ya Jumapili 25.06.2017 uliweza kushiriki ibada ya KUONDOA NJAA iliyofanyika katika hekalu la Mungu la Mlima wa Moto Mikocheni "B". UAMUZI uliofanya wa kuja nyumbani mwa Mungu umekuwa baraka kwa kanisa na mbele za Mungu. Hii inaonyesha ni jinsi gani unampenda Mungu wetu wa mbinguni.
Sio kila mtu aliweza kufika kanisani ila wewe ni kwa NEEMA ya Mungu uliweza kufika kanisani na kuhudhuria ibada ya KUONDOA NJAA iliyotawala majumbani mwetu. Kuna watu waliatamani sana kufika lakini wameshindwa kufika kanisani. Ila wapo wengine walifungwa fahamu zao na shetani na hawakuweza kuona umuhimu wa kuja kanisani, wamebaki majumbani mwao, maofisini mwao, makazini mwao, mitaani na sehemu mbalimbali wakiendelea na shighuli zao za kila siku. Ila wewe uliyebahatika kufika umefanya jambo jema mbele za Mungu na mbele za wanadamu. Kile ulichopokea kanisani kikafanya kazi katika maisha yako na pia ukawagawie na wenzao ili nao washiriki baraka ulizozipata.
Kuna wengi walitamani kusikia Neno la Mungu ambalo leo hii wewe umeweza kulipata kutoka kwa Mungu kupitia mtumishi wake Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na wachungaji wengine kama Mch. Noahl Lukumay na Mch. Francis Machichi, lakini kwao imekuwa ni ngumu kuhudhuria ibada hii. Mshukuru Mungu kwa neema uliyoipata siku ya Jumapili.
Nasi tupo katika maandalizi ya kuandaa somo ambalo lilifundishwa katika ibada ya KUONDOA NJAA siku ya Jumapili 25.6.2017 kwahiyo endelea kufuatilia post zetu na Mungu atakubariki sana.