RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

16.07.2017: WATU WATAOKWA NA ROHO CHAFU WAKATI WAKIBATIZWA SIKU YA JUMAPILI

Hawa ni baadhi ya watu walioamua kubatizwa kwa maji mengi katika ibada ya KUPELEKA MASHITAKA YETU KWA MUNGU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mh. Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 16.07.2017
16.07.2017: MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B": WALIOBATIZWA
Wachungaji waliwaombea kabla ya kuwabatiza kwa maji mengi. wakati wakiombewa baadhi yao walitokwa na mapepo, roho chafu na majini yaliyowatesa kwa kipindi kirefu.

Siku ya Jumatatu na Jumanne walianza masomo yao ya kukulia wokovu masaa ya jioni. Walimu kwa wiki nzima walijipanga kwaajili ya kuwafundisha watu wa Mungu ili waijue kweli na wakishaijua itawaweka huru. 


Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuwahurumia watoto wake na kuwakaribisha katika utawala wake. Pia tunawashukuru wainjilisti wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kila mmoja aliyehusika kuwahamasisha watu hawa kuokoa na kubatizwa. Hii ni hatua kubwa sana waliochukua katika maisha yao, maisha waliyoanza sasa ni mapya na yatakuwa ni maisha ya furaha na mafanikio kwasababu wanaye Mungu atakayewapa furaha na kufungua milango ya mafanikio iliyokuwa imefungwa na adui shetani.


Watu wa Mungu hawa bado wanahitaji sana maombi yako ili wazidi kudumu katika wokovu. Adui shetani anawawinda ili warudi nyuma, lakini tukisimama katika maombi hawezi kabisa kuwapata hawa watumishi wa Mungu. SIMAMA IMARA kumpinga shetani juu ya watumishi wa Mungu.


Yawezekana na wewe umetamani kuokoka, naomba nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.


Ninaamini ukikanyaga katika kanisa hili la Mungu utatoka na muujiza wa afya yakom nyumba yako, kiwanja chako, kibali chako, safari za nje ya nchi yako, mafanikio katika masomo yako, ndoa yenye amani, kupata mume/mke kutoka kwa Mungu na mengine mengi mazuri.


Unapokuja kanisa njoo ukiwa na IMANI kuwa Mungu leo atagusa shida yako na itaondoka katika jina la Yesu Kristo.

























































Comments