Homa ya Ini ni miongoni mwa magonjwa yanayotajwa kuwa hatari sana katika maisha ya binadamu ambapo kutokana na tishio hilo July 28 kila mwaka Dunia huazimisha Siku ya Ugonjwa wa homa ya Ini kwa lengo la kuwatahadharisha watu.
Wataalamu wa mambo ya tiba wanasema watu ambao wako katika hatari ya kupata maambukzi ya ugonjwa wa homa ya Ini ni pamoja na madaktari wanaofanya upasuaji kwa kuwa ugonjwa huo huambukizwa kwa njia ya damu.
Taasisi ya Tanzania Hepatitis Free Community imeanza kujitolea kufanya vipimo vya ugonjwa wa homa ya Ini kwenye Hospital ya Sekou Toure, Mwanza ili kuwa sehemu ya kutoa elimu ya namna ya kujikinga nao.
Comments