20.08.2017: MANENO MAZITO ALIYOHUBIRI BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE SIKU YA JUMAPILI YAGUSA WALIO WENGI
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 20.08.2017 katika ibada ya “KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA NA MAADUI ZETU TUSIFANIWE alikuwa na haya ya kusema kwa waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”, alianza kwa kusema, “Najua umechoka,najua unaumwa, najua unashida,najua umekwama mahali. Lakini leo upo nyumbani kwa BWANA na ndio mahali pakufunguliwa huwezi kuondoka bila kufunguliwa hata kama tutakuwa na Neno la Mungu lakini nilazima kwanza ufunguliwe kwanza, uwekwe huru, moyo wako uweze kuwa wazi, uuone ukuu wa Mungu. Na Mungu hauwezi kumuona akitembea na suti ,akitembea na kanzu utamuona Mungu kwa matendo yake makuu. Mungu akutane na wewe leo ,Mungu akutane na haja ya moyo wako leo,Mungu aondoe shida zako leo. Ukipata muda soma Isaya:33:24 , Hakuna mtu katikati yenu ataye sema mimi ni mgonjwa watu wakaao humu wata samehewa uovu wao.
MUNGU ANACHUKIA KUSIKIA UKILALAMIKA NA KUUMIA
Bwana asifiwe sana, Mungu wetu anaumia na masikio kusikia mtu anasema anaumwa mgongo,kichwa, tumbo au ni dhaifu kwa magonjwa mbalimbali. Wengine wanaishi maisha ya hofu pengine kutokana na sukari kupanda au pressure kupanda. Mungu anachukia kusikia malalamiko, masikitiko na kilio mbele ya watoto wake kwasababu Yeye amesema katika kutoka :15:26 “Mimi Mungu ni Mungu niwaponyae na magonjwa yenu yote”. Siku hizi kila nyumba inalia, kila mtaa unalia kutokana na magonjwa mbalimbali yanayowasumbua. Utakuta mgonjwa amepelekwa hopitalini na kufanyiwa matibabu yote lakini bado ugonjwa umeng’ang’ania na wengine wanaenda hospitalini kwa matibabu lakini daktaria anasema haoni uogonjwa. Watu wa namna hii wamefungwa na nguvu za giza, wamelogwa, wametupiwa majini, wamesemewa maneno mabaya katika afya zao. Lakini leo nina habari njema kuwa Mungu ataondoa magonjwa yote, shida zote, maumivu yote, mapepo yote, majini, malalamiko na manung’uniko yote katikati yetu kwasababu yeye ni Mungu atuponyae na magonjwa yote. Nataka kukuambia rafiki yangu upo mahali sahihi furahia mchungaji wako anaingia akilini mwako na roho yako kabla hauja ingia mbinguni nilazima uishi duniani kwa amani na bila mateso kwasababu wewe ni mtoto wa Mungu na unafuta maagizo yake anayotuagiza katika kitabu chake kitakatifu yaani Biblia. Ukitaka maisha ya amani basi tenda mema, uwe na upendo kwa kila mtu, acahana na dhambi.
ANGALIA WOKOVU WAKO KAMA UTAKUFIKISHA MBINGUNI, AMUA KUOKOKA KWA KUMAANISHA
Alisema duniani mnayo dhiki lakini jipeni moyo mimi Mungu nimeushinda ulimwengu na ninyi mtaushinda .Ulipookoka ukuahidiwa kuwa utakuwa na maisha bora, lakini unashangaa kuona bado maisha yako ni dhaifu kifedha, kiuchumi, kiafya n.k Hii inatokana na wokovu ulionao, unatakiwa kujichunguza kwa makini na kujiuliza hivi kweli umeokoka au unajiita mlokole wakati hufanyi yaliyo ya walokole. Unapookoka maanisha na usiwe mtu wa kujifanya umeokoka wakati unatenda maovu mengi. Kama utajiita umeokoka wakati ni mwovu, nakuambia hutaona mbingu na utazidi kuteseka duniani. Amua kuokoka na kutenda yale Mungu akuagizayo.
HESHIMU MIKUTANO YA MUNGU
Kama umekuja kumwabudu Mungu kanisani kwa Roho ya kweli, hutatoka kama ulivyoingia kwa jina la Yesu Kristo, ni lazima Mungu afanye jambo katika maisha yako. Mkutano unaofanyika katika nyumba ya BWANA si kama mikutano ya siasa, bali ni kusanyiko la watu wa Mungu wenye nia moja ya kwenda mbinguni. Mikutano ya kisiasa unaweza kuhudhuria na ukutoka bure na pengine kutoka na majeraha kwasababu sio mkutano unaomtangaza Kristo, mkutano wa Mungu sio mkutano wa kikao cha harusi bali ni mkutano wa Mungu mwenyewe, yeye yupo hapa anatenda kwa ishara na miujiza kwa walio wake. Yesu Kristo aliyemfufua Razaro yupo katikati yetu, yeye aliyekausha bahari ya shamu yupo katikati yetu atakausha magonjwa yako yote, masikotiko yako yote, atakausha machozi yako yote,taabu za kila aina zitakoma.
MUNGU ANASEMA, “ATAKOMESHA SHIDA ZAKO”
Ukisoma Hagai :1:9 inasema, “Unawaza nini juu ya BWANA? Mimi ni Mungu, nitakomesha misukosuko yote na hautaiona tena.Unajua tunampenda Mungu kwasababu ni Mungu mwenye vyote unaweza kwenda kwa specialist wanasema huyu ni daktari bingwa wa moyo, huyu ni daktari binwa wa mifupa ,huyu ni daktari bingwa wa macho anaweza akashindwa lakini yeye YesuKristo ni daktari wa vyote katika jina la Yesu Kristo.Wale ambao wamekawia kupata watoto watapata katika jina la Yesu maana yeye ni vyote ndani ya vyote yeye aliumba tumbo la uzazi la mwanamke anauwezo wa kulikarabati yeye ana uwezo wa kuizibua mirija huyu mama akapata mimba.Haleluya!Bwana asifiwe! Anasema wala hakuna mwenyeji wenu atakaye kuwa na manung’uniko wala atakaye kosa usingizi akisema mimi naumwa niwashieni feni ,niwashieni feeeeni watoto kama wapo mbali baba washa feni mwenzio shetani ameshindwa kwa jina la Yesu.
MUNGU ANAWEZA KUPONYA UGONJWA WAKO USIOONEKANA NA MADKATARI
Kuna shirika linaitwa World Health Organisation (WHO) limekuwa likitusaidia sana katika maswala ya afya zetu pamoja na magonjwa tunayokumbana nayo lakini kuna magonjwa mengine yana majina na mengine hayana majina. Lakini Mungu anaweza kuponya magonjwa yasiyo kuwa na majina na yenye majina. Kuna magonjwa mengine unaenda hospitalini unaambiwa hawayaonekani wakati wewe unaumwa sana, kila wakikupa dawa hazifanyi kazi kabisa. Nataka nikwambie ya kwamba Mungu anaweza yote kwani yeye ndiye aliyetuumba na anajua “system” nzima ya miili yetu. Unapokuwa na huyu Mungu kwa kumaanisha na kufuata maagizo yako, hutakumbwa na magonjwa kabisa. Kuna magonjwa mengine ya kututishia, watu wanasema eti ngoja ukitumbua kipele katika ngozi yako ni kosaa, ukiweka kwenye maji kipele kinaota, ukijikuna kwenye kichwa kipele kinaota.
MNG”ANG”ANI YESU ILI UPONYWE NA MAGONJWA YAKO
Aliye ndani yetu ni mkuu kuliko aliye ulimwenguni. Shetani ataleta magonjwa lakini hata tuweza hatuta achana na Yesu kwasababu ya magonjwa tutang’ang’ana na Yesu siku zote. Leo nataka tushughulikie ugonjwa ulio kuvamia, umekuwa ukiteseka na magonjwa, unahangaika huku na kule bila ya mafanikio, lakini leo Yesu anakwenda kukuponya kama utamkubali na kufuata njia zake njema. BWANA alichukua magonjwa yote msalabani na kwakupigwa kwake sisi tuwazima.
Kupitia maombi utakayaomba hapo ulipo siku leo utaona maajabu makuu ya Mungu akitenda katika maisha yako. Kama mtumishi wako Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la watumishi wa Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni “B” leo tutakwenda kuingia katika mwili wako tuweze kuponya ugonjwa unaokusumbua tutang’oa kila pando lisilo pandwa na Mungu .Bwana anasema kila pando lisilo pandwa na Mungu Mathayo:15:13 litang’olewa ugonjwa huo haukupandwa na Mungu ulipandwa na shetani tuung’a kwa jina la Yesu. Leo utaondoka ukiwa mzima kwa jina la Yesu. Shida nyingi katika nyumba ni magonjwa watu wanakwenda mpaka India, South Africa kutafuta uponyaji kwasababu watu hawa wamehangaika katika hospitali za nchini mwao hawakuweza kupata uponyaji, wamehangaika kwa waganga na makanisa mbalimbali lakini bado wanateseka na magonjwa, lakini leo nakwambia kwamba nakupeleka kwa daktari bingwa wa kila magonjwa ambaye ni Yesu Kristo ambaye atashuka ili aweze kukuhudumia. Mwngine anaweza kusema kwani mimi naumwa sana na siponi wakati wenzangu wakiumwa tu wanaponya mara moja. Unatakiwa kuwa karibu na Mungu.
UNAPOTENDEWA NA MUNGU USIACHE KUSHUHUDIA
Ukipata mafundisho basi uwe msaada kwa watu wengine sio umefundishwa na unabaki nayo mafundisho, na unapoponywa na Mungu usikae kimia bali washuhudie na wengine ili imani zao zikue. Utakuta watu wengine wameponywa na Mungu utashangaa wanajikausha, hawashuhudii kwamba wamepona. Unapotendewa usikae kimia kwasababu wewe ni faraja kwa watu wengine wanaopitia mapito magumu kama yako au zaidi yako. Mkumbatie anayeumwa, mbebe mwenye shida, msaidie mtu aliyekwama utaona hapo Mungu anatenda katika maisha yako .
Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare..
Mlima wa Moto Mikocheni "B"
Ibada ya Jumapili hii ni saa 3 asubuhi hadi saa 8
Njoo na rafiki/ndugu yako
Usafiri bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, baada ya ibada utarudishwa kituoni
Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
Comments