27.08.2017: MARTHA KOMANYA AKONGA MIOYO YA WATU WALIOFIKA KATIKAIBADA YA TAMASHA LA MAOMBEZI Hakuna mtu asiyetamani kusifiwa, hata wewe unatamani kuona w
Mungu wetu ni Mungu wa sifa. Katika vitu anavyopenda Mungu wetu ni pamoja na KUMSIFU kwa mambo yake makuu anayoyatenda kwa viumbe na mime yake. Mungu alikuumba ili umtumikie na ni pamoja na kumsifu kwa yale anayokutendea katika maisha yako. Kuna vitu vingi sana Mungu anafanya katika maisha yako na vimefanyika baraka katika familia yako au jamii yako inayokuzunguka.
atu wanakusifia kwa kile unachofanya katika maisha yako. Siku ya Jumapili 27.08.2017 mtumishi wa Mungu Martha Komanya ambaye pia ni mzee wa kanisa na mwimbaji wa Praise & Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" aliyejaa upako wa tofauti katika huduma yake ya uimbaj, alitubariki sana kwa nyimbo zenye kutufundisha, kutuburudisha na kutuadibisha na kutufariji kwenye kipindi cha kusifu. Kipindi hiki kilifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" katika ibada ya Tamasha la Maombezi. Baada ya kumalizika kwa kipindi hiki watu waliweza kusikiliza Neno la Mungu na baadaye kuingia katika ibada ya Tamasha la Maombezi.
Kupitia kipindi cha sifa watu walifarijia, walibarikiwa, waligiswa na nguvu za Mungu, waliinuliwa imani zao, waliadishwa kwa ujumbe mzito uliokuwa ukitolewa na waimbaji.
Jitahidi sana kuwa na mazoea ya kutenga muda kidogo wa kumsifu Mungu kwa njia ya uimbaji au kutamka maneno kutoka ndani ya moyo wako kwa yale aliyokutendea na yale ambayo unatarajia kukutendea. Hata ukiwa kazini, nyumbani, safarini, shambani, au mahali popote pale, jitahidi kuomba kibali kutoka kwa Mungu akupe muda kwaajili ya kumsifu na kumtukuza.
Unatakiwa kukumbuka kuwa itafika wakati utashindwa hata kuimba au kumsufu Mungu kutokana na majaribu utakayokumbana nayo kama vile ugonjwa, uzee (kikongwe) na mrngine kama hayo. Kama utakuwa unaimba usiogope watu watakucheka kwa sauti yako mbaya, ila wewe muangalia Mungu juu na kumtukuza. Shetani anaweza kukushauri na kusema, "Hiyo sauti yako ni mbaya", na akakuletea watu wa kucheka wakati ukiimba. Jiamini kwasababu unajua unayemtumikia.
Wewe uliyekosa kufika katika ibada hii tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana
Martha Komanya
Comments