27.08.2017: MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIVYOWAOMBEA WAUMINI WAPYA WALIOAMUA KUOKOKA SIKU YA JUMAPILI
Tuna kila sababu ya kukupongeza wewe uliyeokoka siku ya Jumapili 27.08.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kuongozwa sala ya toba. Uamuzi wako wa kuokoka umekuondoa katika mateso uliyokuwa ukipitia kwa muda mrefu kabla ya kuokoa, ni hivi sasa umekombolewa kama alivyokombolewa Paulo (Wafilipi 1:19). Umekombolewa Kiroho na kuÄanzia sasa unauhakika wa kuingia mbinguni kama hautatenda dhambi tena. Wewe umeokolewa kutoka kwa "ghadhabu," yaani, hukumu ya Mungu (Warumi 5:9, 1 Wathesalonike 5:9). Dhambi yako iliyokutenganisha na Mungu kwa sasa haipo tena (Warumi 6:23). Mungu tu ndiye aliyeweza kuondoa dhambi na kuwaondoa na adhabu ya dhambi (2 Timotheo 1:9, Tito 3:5). Hivi sasa Mungu amekuokoa kwa njia ya Kristo (Yohana 3:17), umeokolewa kwa imani, kwahiyo ni lazima uisikie injili - habari njema ya kifo cha Yesu na ufufuo wake (Waefeso 1:13). ni lazima mumwamini -kikamilifu Bwana Yesu (Warumi 1:16) katika maisha yako yote. Unatakiwa kujua kuwa " Ukombozi unapatikana katika Yesu peke yake (Yohana 14:6; Matendo 4:12) na Mungu anategemewa kuutoa, uhakikisho na usalama.
Usikose mafundisho ya kukulia wokovu siku ya Jmatatu hii na Jumanne katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 9 mchana na kuendelea. Watumishi wa Mungu wamejipanga kukusaidia.
Siku ya Jumapili ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 98 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa, utaona magari yetu. Baada ya ibada utarudishwa kituoni.

Comments