RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

App maalumu kuzinduliwa China, unakodi Mlinzi kwa Tsh. 22,000 kwa saa



Najua wapo watu wangu ambao wanapenda na wanafuatilia masuala ya Sayansi na Teknolojia ambayo kila siku yamekuwa yakichukua headlines sehemu mbalimbali duniani kwa kufanya ugunduzi wa mambo.

August 22, 2017 ninayo hii ambayo unaambiwa kuna good news imetangazwa kwa watu wanaohitaji usalama wanapokuwa katika hali ya hatari.

Kampuni moja katika mji wa Qingdao, China inatarajia kuzindua app mwezi ujao ambayo itawawezesha watu kukodi walinzi wao binafsi ambapo unaambiwa bei itakuwa ni kati ya yuan 70 hadi 200 ambazo ni pound 8.15 hadi 23.38, sawa na Tsh. 22,000 hadi 64.400 kwa saa.

Inaelezwa kuwa app ambayo imeanzishwa kwa ushirikiano kati ya kampuni ya Qingdao Aladdin Group na kampuni ya ulinzi itaanza rasmi kutumika mwezi ujao ikiitwa Jinyiwei.

Mmoja wa wataalamu wa app hiyo Li Shangshang, aliuambia mtandao wa China Daily:>>>”App imewaunganisha zaidi ya maafisa 50,000 wa ulinzi katika makampuni 47. Upatikanaji wao utaoneshwa kwenye ramani ya app katika muda halisi.”

Walinzi wote watapewa mafunzo maalumu na watatakiwa kuvaa sare wakati wanafanya kazi ambapo Li alisema: “Ambao watajihisi hawatokuwa salama, hasa wakati wanakwenda sehemu fulani au kubeba vitu vya thamani.”

Comments