ZABURI 135: 1-3: "Haleluya. Lisifuni jina la BWANA, enyi watumishi wa BWANA, sifuni. Ninyi msimammao nyumbani mwa BWANA, nyuani mwa nyumba ya Mungu wenu. Msifuni BWANA kwa kuwa BWANA ni mwema, liimbieni jina lake kwa maana lapendeza."
Inabidi ufike wakati utenge muda wako kwaajili ya kumsifu tu Mungu wako kwa njia ya uimbaji au kutamka maneno (kwa kuongea). Tafuta maneno mazuri ya kuongea na Mungu wako kwa kumsifu kwa yale unayoona yamefanyika katika familia yako, ofisi yako, kazi yako, biashara yako, afya yako, shambani kwako, marafiki zako, mume/mke wako, mchumba wako, na kila sehemu ambayo unahusika. Mwambie Mungu maneno matamu kutoka moyoni mwako kwa KUMSIFU.
Unajua kila mtu anapenda kusifiwa, mimi binafsi natamani kuona mtu akinisifia kwa vile vitu ninavyofanya. Na ndio maana unaona watu wanapenda kufanya makubwa katika jamii ili wasifiwe na wawe salama katika maisha yao. Watu wapo busy na kujiremba au kupendeza ili wasifiwe na wengine. Na Mungu wetu anapenda kuona wewe unaacha kazi zako zote na kutenga muda kwaajili ya KUMSIFU kwa yale anayokufanyia. Mungu wetu ni Mungu wa sifa na kama ni Mungu wa sifa tuna kila sababu ya KUMSIFU.
Ni vyema ukajitakasa kabla ya kuanza kumsifu Mungu wako, Tubu dhambi zako ili utakapoanza kumsifu Mungu wako unakuwa huru kwasababu huna doa la dhambi ndani yako. Unatakiwa kumsfu kutoka ndani ya moyo wako na sio kwa kuiga watu.
Unapokuwa kanisani ukimsifu Mungu wako, fanya kutoka ndani ya moyo wako yaani maanisha. Usianze kumsifu Mungu wako kwa mazoea au kwa kutomaanisha.
Tunakushukuru wewe uliyeabudu nasi katika ibada ya MAOMBI YA KUFUFUA VITU VYETU VILIVYOKUFA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 17.09.2017. Tulimuona Mungu akishughulika nasi katika kipindi cha kusifu kilichoongozwa na PRAISE & WORSHIP TEAM ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tuliona Mungu akiachilia nguvu zake kupitia sifa.
Wewe ambaye hukufika, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kanisa limeandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa. Ukifika hapo utasikia watu wakisema kanisani kwa Mama Rwakatare. Baada ya ibada utarudishwa kituoni. Mlete na mwingine. Ubarikiwe na BWANA

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
Comments