29.10.2017: MANENO MAZITO YA MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE KUHUSU UJIO MWINGINE WA KONGAMANO LA SHILO TANZANIA 2017 AMBALO HUFANYIKA MARA MOJA KWA MWAKA.
Katika ibada ya KUTENGUA MANUIZO NA LAANA KATIKA MAISHA YETU
iliyofanyika siku ya Jumapili 29.10.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto
Mikocheni “B”, Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kufungua rasmi
KONGAMANO LA SHILO TANZANIA 2017 na alikuwa na haya ya kusema, “Bwana Yesu
asifiwe…Katika kitabu cha 1 Samweli 3:21 kinasema, “Nae BWANA akaoneka tena
huko Shilo kwakuwa BWANA akajifunua kwa Samweli huko Shilo kwa Neno la BWANA,
nalo neno la Samweli likawajia Israel wote.”
Shilo ni kongamano kubwa la watoto wa Mungu au tunasema ni
mkutano mkubwa ambao hufanyika mara moja kwa mwaka au ni kongamano au mkutano
wa Mungu wa kuoneka tena kwa watoto wake. Katika Biblia inasema kipindi cha
nyuma Mungu alikuwa anaonekana kwa wakati lakini watoto wa Mungu walipokuwa
wakikutana kipindi cha Shilo, Mungu aliweza kuonekana kwao tena.
Wana Mlima wa Moto tunasema kuanzia tarehe 3 hadi 10/12/2017
kwa wiki nzima kutakuwa ni kongamano la watoto wa Mungu. Lengo la kongamano la
Shilo Tanzania 2017 ni KUHAKIKISHA MUNGU ANATEMBEA NA KUONANA NA WATOTO WAKE
lakini zaidi sana kukagua maisha ya watoto wake.
Umeteseka vya kutosha kwa mwaka mzima, umeugua, umepata
misukosuko mikubwa na midogo, lakini wapo waliolewa, waliopata magari, viwanja,
nyumba, kazi, waliosafiri nje ya nchi, waliofanikiwa n.k, kwahiyo kwa wiki
nzima tutafanya sherehe kwaajili ya shukrani kwa kwa Mungu kwa wema na fadhili
zake jinsi alivyoweza kututetea.
Lakini bado Mungu anataka kukagua maisha yako kwa mwaka
mzima uliokuwa nao. Kwa mwaka mzima umekwama wapi, umepita katika magumu yapi,
unadaiwa na akina nani, kwanini uliugua magonjwa mbalimbali na mabo mengine
kama hayo. Mungu anataka kuingilia kati katika magumu ya maisha yako ili uweze
kuwa huru kwelikweli.
Wakati wa Shiloh ni wakati mzuri wa kuangalia kile ambacho
kimetoka katika maisha yako. Kama wanadamu tumepita katika mambo mengi kama
vile changamoto za kiuchumi, kiimani, kifamilia, kikazi n.k, sasa BWANA anataka
kutunyunyizia maji tena katika ukame tuliokuwa nao kwa mwaka mzima.
Wakati wa SHILOH ni wakati wa kufunguliwa kwako. Nyakati
hizi huwa ni nyakati za miujiza. Huu utakuwa ni mkutano wa UHAMUSHO na MIUJIZA.
Kila kitu kilichokuwa kigumu kwa mwaka mzima, BWANA anataka kuingia mzima
mzima-ngi…ngi…ngi…ngi…ngi…kukuondoa katika hali ngumu uliyopitia na unayopitia
kwa sasa. Mungu ni kama baba yako uanavyowahurumia watoto wake, Naye anataka
kukuhurumia wewe kama mtoto wake.
Unajua watu amabao hawajaokoka wao wana waganga wa kienyeji
ambao huwasaidia kutatua matatizo yao lakini baadae hukumbwa na makubwa, ila
sisi tuliokoka wakumkimbilia ni Mungu wetu wa mbinguni na kama tunamtegemea
Mungu basi fungua moyo wako kipindi hiki cha SHILOH ili Mungu aingie ndani yako
na tuone mabadiliko katika maisha yako.
Kwa mwaka mzima umeteseka, Je, unataka na mwaka huu uteseke
jamani? Tunataka kuona mabadiliko katika maisha yako. Tunataka haja ya moyo
wako ikapate kutimia kwa jina la Yesu, tunataka madeni yako yakafunguliwe na
Mungua akakubariki kwa jina la Yesu, yaliyokuwa magumu yakawe mepesi kwako kwa
jina la Yesu.
Ninaona miujiza ikija kwako kwa jina la Yesu, ninaomba Mungu
akafute kila mateso, masikitiko, huzuni inayokuumiza kwako kwa jina la Yesu.
Mungu atatenda jambo jipya kwaajili yako.
Pokea pesa kwa jina la Yesu, pokea Baraka zako, leo ni
mwisho wa madeni yako, magonjwa, masikitiko, kwa jina la Yesu. Mungu anashuka
na anakutana na kila mmoja kwa jina la Yesu.”
Pia tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii kuanzia saa
3 asubuhi hadi saa 8 mchana hapa Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Kutakuwa na
usafiri bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa
barabara ya Coca Cola. Baada ya ibada kumalizika utarudishwa kituoni.
Comments