Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa kwa dalili anazoziona kwa serikali ya awamu ya tano muda si mrefu itafungia mitandao ya kijamii.
Mchungaji Msigwa amesema hayo baada ya serikali kufungia moja ya gazeti jana na kusema kuwa serikali ya awamu ya tano imekuwa haipendi kukosolewa katika mambo mbalimbali hivyo anaona kabisaa serikali itafungia mitandao hiyo ya kijamii kwa kuwa imekuwa ikitumika sana na watu ambao wanatoa mawazo yao mbadala, kukosoa na kuchapisha taarifa mbalimbali ambazo zinaoeneka kutowafurahisha baadhi ya viongozi.
“Kwa serikali hii isiyopenda kukosolewa, naanza kuona kwa mbaliii kufungwa kwa mitandao ya kijamii. Waoga sana hawa” aliandika Peter Msigwa kupitia mtandao wake wa Twitter.Viongozi mbalimbali na wa upinzani nchini wamekuwa wakitumia sana mitandao ya kijamii kama njia ya kuikosoa serikali, kuishauri na kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii.
Comments