TAFAKARI:
"Hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho. Yohana 6:44"
Katika ibada ya KUTAMBUA NGUVU YA MUNGU ILIYOMO NDANI YA MUAMINI iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Siku ya Jumapili 26.11.2017, kuna watu wengi sana walijitokeza katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakihitaji kubarikiwa na Mungu kwa kuchukua bahasha za kuchangia Kongamano la SHILO Tanzania 2017 pamoja na sticker zilizoombewa na mtumishi wa Mungu Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare pamoja na jopo la wachungaji wa kanisa hilo. Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare naye aliwezxa kuchukua sticker yake na kubadika katika Biblia yake.

Watu waliweza kuchukua bahasha hizo kwaajili ya kusapoti kazi ya Mungu ili isonge mbele. Kupitia kongamano la SHILO watu wengi hupokea miujiza yao na hushuhudia kile ambacho Mungu amewatendea katika maisha yao. Pia watu wengi huokoka na kubatizwa.
Kumbuka kongamano la Shilo litaanza rasmi siku ya Jumapili 03 hadi Jumapili 10 Desemba 2017 ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Katika kongamano hili hakuna kiingilio.
Kwahiyo usikose kongamano hili la SHILO ambalo siku ya Jumapili litaanza saa 3 asubuhi na katikati ya wiki litaanza saa 9 alasiri,
Kanisa limeandaa uasafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
Comments