Dismas Mbawala na mke wa Joyce waliweza kumtolea Mungu sadaka ya shukrani kwa kuwafanikisha kupata elimu yao “masters”. Wakishuhudia katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” katika ibada ya maandalizi ya mkesha wa Krismasi Jumapili 24.12.2017, Bwana Dismas Mbawala alikuwa na haya ya kusema. “Bwana Yesu asifiwe, nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa yale aliyotutendea na mke wangu Joyce. Kabla sijaendelea naomba ushiriki nami kwa kusoma Zaburi 111:1-3.
Hakika tuna kila sababu ya kusimama katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” tukisema Mungu ametutendea na kutoonekania katika masomo yetu. Nakumbuka Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa akisema “Pokea Mafaniko katika masomo yenu”, na sisi tukiwa hapa kanisani tulikuwa tukipokea kwa imani. Ilikuwa siku ya Ijumaa 22.12.2017 mimi na kipenzi changu Joyce tume-graduate degree masters kwa pamoja katika chuo cha Mzumbe. Mimi Dismas Mbawala nime-geaduate Masters of Science and Human Resource Management ambapo mke wangu ame-graduate Masters of Business Administration and Corporate Management.
Ninakumbuka kipindi cha nyuma nilikuwa namtembelra Naibi Waziri Kilimo Mhe. Mary Mwanjelwa (MB) akiwa anafanya kazi katika kampuni ya PSI kabla hajawa Naibu Waziri alikuwa ananitia moyo na nilikuwa nafurahi sana kumuona akifanya kazi huku akisoma, hakika “she was motivated me”,hakika niliona hata mimi na mke wangu tunaweza kuwa kama yeye.
Ninamshukuru sana Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kututia moyo na kuniombea mpaka leo tumevuka. Pia nawashukuru wazee wa kanisa, wachungaji wa kanisa hili.
Baada ya Bwana Mbawala kutoa shukrani zake, mke wake Joyce alikuwa na haya ya kusema. “Ninawasalimu katika jina la Yesu. Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ninakushukuru sana kwa upendo wako, watoto wako tulikuwa tukipotea hapa kanisani na hatuonekani kwaajili ya masomo, lakini ulishika simu yako na kutupigia kutaka kujua maendeleo yetu. Ninawashukuru sana wazee wa kanisa kwa maombi yenu na ninawapenda. Upendo mlioonyesha kwetu ninaomba muendelee kuonyesha na kwa wengine. Nina washukuru pia wachungaji kwa maombi yenu, Mch. Mama Lucas umefanyika Baraka kubwa sana kwangu. Mungu awabariki sana.
Naibi Waziri Kilimo Mhe. Mary Mwanjelwa (MB)
Comments