24.12.2017: MCHUNGAJI KUTOKA KEN YA AMKIMBILIA MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE KUWEKEWA MIKONO AANZE KUHUDUMU RASMI
Mchungaji kutoka Kenya mabye alishawahi kufanya kazi katika shuke za Kimataifa za St. Mary's ambazo zinamilikiwa na Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa na haya ya kusema na kumshukuru Mungu, "Ninamshukuru Mungu kwa kunileta mahali nilipolelewa kiroho Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Nilianza kumjua Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare nikiwa na miezi miwili tangia nimeokoka, naye aliweza kunishikiria na kunielekeza njia sahihi ya kukulia wokovu. Nakumbua kipindi cha nyuma nilikuwa sijaokoka sawa sawa, nilikuwa naiga tu watu lakini Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kujitoa kunifundisha neno la Mungu kwa undani pamoja na ile tabia ya kuwa mtoaji kanisani.
Baada ya kukomaa katika wokovu nilienda Kenya. Nikiwa huko nikawa nasali katika kanisa moja. Bishop wangu wa Kenya akawa ananambia sasa na weza kuanza huduma, lakini mimi nikawa nakataa, nikimwambia siweze kuhubiri mpaka nimekutana na mama yangu wa Kiroho Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ili anipe baraka zake. Ninamshukuru Mungu kwa siku ya leo kwa kunileta kanisani Mlima wa Moto Mikocheni "B" kukutana na Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ili anipe baraka katika huduma yangu ya kuhubiri.
Pia Mungu amenibaraki nimepata mke mzuri na tumefanikiwa kuwa na watoto."
Hivi ndivyo mtumishi wa Mungu kutoka KENYA alivyomshukuru Mungu kwa yale aliyomfanyia katika maisha yake.
Yawezekana unatamani kuwa mchungaji au kufanya kazi ya Mungu na kila ukiamua kufanya unaona kuna nguvu zinakuzuia au unasikia sauti katika nafsi yako ikisema huweza kufanya kazi ya Mungu. Tunakukaribisha Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ukutane na nguvu za Mungu kupitia mtumishi wake Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, atakuombea na kukutamkia baraka katika huduma yako.
Kanisa limeandaa usafiri wa bure wa kufika kanisani kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Utaona magari yetu. Baada ya ibada utarudishwa kituoni.
Comments